Monday, August 25, 2014

Watu-samaki (Fishmen)

Mtu-samaki (Fishman)

Watu-samaki ni wanachama wa mbari ya kiamfibia iliyo karibu kufa ambayo iliishi wakati wa enzi ya Devonia walio na uwezo wa kupumua ndani na nje ya maji. Wao hudhuriwa na rotenoni na nuru ya kung’aa (kutokana na mazingira yao yenye maji machafu), huwa na mikono yenye utando na kucha kali na ngozi ngumu yenye magamba ya kijani-samawati ambayo ikiunganishwa na kipengele chao cha kujiponya huwawezesha kunusurika majeraha ambayo yangekuwa hatari kwa binadamu, kama vile mipigo ya bunduki na kuuliwa kwa kuchomwa. Viumbe hawa huwa na jozi ya mapafu yasiyotumika kwa muda iwapo mayavuyavu yao yataharibika kupita kiasi. 35% ya watu-samaki imetengezwa kwa chembechembe za damu nyeupe zinazokosa kiini. 

Fish-men are members of a nearly extinct amphibious race that lived during the Devonian age, capable of breathing both in and out of water. They are vulnerable to rotenone and bright light (due to their murky water habitat), have webbed hands with sharp claws and tough scaly greenish-blue skin, that with their combined healing factor allows them to survive wounds which would be fatal to humans, such as gunshots and full immolation. These creatures have a dormant set of lungs, in case their gills become irreparably damaged. 35% of fish-people’s blood is composed of white corpuscles lacking a nucleus. 

Kiumbe kutoka Wangwa Mweusi (The Creature from the Black Lagoon)
Kiumbe hiki kutoka wangwa mweusi ndiye mwanachama wa mwisho anayejulikana kuishi katika mbari ya amfibia walio na umbo la binadamu. Mtu-yavuyavu aliyegunduliwa na kupewa jina na Dkt Thompson miaka ya 1930 aliishi katika wangwa ulioko katika eneo pana isiyotafitiwa ya Msitu wa Mvua wa Amazoni. Karibu nusu-karne baadaye, wenyeji wa msitu wa mvua walidai kuwa wameona mtu-samaki mwingine mwenye mapezi ya nyuma mapana yenye rangi ya kaharabu akiishi kwenye maji machafu.

The creature from the black lagoon was the last known surviving member of this race of humanoid amphibians. The gill-man, discovered and named by Dr. Thompson in the 1930s, dwelled in a lagoon located in a largely-unexplored area of the Amazon Rainforest. Almost half a century later, the rainforest natives claimed to have seen another fish-man with large amber-colored dorsal fins inhabiting the murky waters.

No comments:

Post a Comment