Monday, August 25, 2014

Baharia Uranasi (Sailor Uranus)

Baharia Uranasi (Sailor Uranus)
Baharia Uranasi ni mwenye nguvu zaidi wa Skauti-Baharia wote. Yeye ni mtumiaji kitara stadi, dereva mjuzi wa mashindano ya magari, huwa katika klabu ya riadha na kucheza piano ikiambatana na maonyesho ya fidla ya mpenzi wake. Ingawa yeye ni mzuri zaidi katika darasa lake la kwata, yeye ni mbaya zaidi katika darasa lake la lugha ya Kijapani. Yeye huchukia sana nattou (soya iliyochachuka). 

Sailor Uranus is the strongest of all the Sailor Scouts. She is a skilled fencer, professional racecar driver, belongs to the track-and-field club and plays piano in accompaniment during her lover's violin performances. Although she is best at her physical education class, she is the worst in her Japanese class. She absolutely hates nattō (fermented soybeans). 

Dunia, Tetemeka! (World Shaking!)
Licha ya Uranasi kuwa mungu wa mbingu, Baharia Uranasi anaonekana kuwa na nguvu nyingine za ardhi kama vile shambulizi lake: “Dunia, Tetemeka!” ambayo duara ya dhahabu ya nishati yenye umbo la sayari ya Uranasi hukusanyika kwenye mkono wake huku akibaniza nishati, akitia ufa ardhini kutupa wimbi la kishindo ya utetemeko upande zote. 

Despite Uranus’s being the god of the sky, Sailor Uranus seems to have some earth-based powers as well, such as her attack: “World, Shake!” where a golden sphere of energy shaped like the planet Uranus gathers in her hand as she slams the energy down, cracking the ground beneath her and sending out a seismic shockwave in all directions. 

Upanga wa Anga (Space Sword)
Yeye ndiye hubeba upanga wa anga, mojawapo wa hirizi tatu za kisasili inayobebwa tu na wale walio na fuwele ya moyo safi. Wakati anapoita nguvu za upanga, ubapa wake unaonyooka huwa inang’aa na angezungusha upanga huo ili kutoa mawimbi ya nishati ya dhahabu kuharibu shabaha yake.

She is the bearer of the space-sword, one of the three mythical talismans bore only by those with a pure-heart crystal. When she summons the sword’s power, the extendable blade would glow and she would swing the sword to release of wave of golden energy to destroy the target.

No comments:

Post a Comment