Friday, May 27, 2011

Awamu za Maada (Phases of Matter)

Awamu za maada (Phases of matter)

Awamu ya kuyeyukaMelting
GesiGas
Hali kiowevuLiquid state
Hali mangoSolid state
Hali ya gesiGaseous state
KiowevuLiquid
MangoSolid
MchanganyikoFusion
MgandishoSolidification
MtoneshoCondensation
MvukizoEvaporation
UsafishajiSublimation

Muundo wa Atomu (The Structure of an Atom)

Muundo wa atomu (The structure of an atom)

Chembebatili (Nyutroni)Neutron
Chembechanya (Protoni)Proton
Chembehasi (Elektroni)Electron
NyukiliaNucleus

Thursday, May 26, 2011

Nyangumi (Whale)

Nyangumi mwenye mfupanyangumi (Baleen whale)
Nusuoda ya nyangumi wakubwa (Mysticeti)

Bamba la kuzuia majiSplashguard
KitovuUmbilicus
KwapaAxilla
Mashimo ya kutolea hewaBlowholes
MfupanyangumiWhalebone (Baleen)
Mifuo ya kooThroat pleats
Mkato wa katiMedian notch
Mkia wa nyangumiFluke
MkunduAnus
Nundu za mgongoniDorsal ridge
Pezi la mgongoniDorsal fin
PuaRostrum
Shina la mkiaCaudal peduncle
Ufa wa ogani za uzazi na mkojoUrogenital slit
VikonoFlippers
ViweleMammary glands

Kinyamadege (Platypus)


Kinyamadege (Duckbilled platypus) ni mamalia Australia aliye na mdomo wa bata, miguu yenye utando kati vidole kama ya fisi-maji na mkia kama wa biva. Ni mmoja wa spishi mbili za mamalia atagaye mayai.

Manyoya ya kahawiaBrown fur
Mdomo wa bataDuckbill
Miguu yenye utando kati ya vidoleWebbed feet
Mwiba mwenye sumuVenomous spike
Nyufa ndogo za masikioTiny ear slits
Tundu za pua ziwezazo kufungwaCloseable nostrils

Oda ya Mamalia watagao Mayai (Monotremata)

Mamalia atagaye mayai (Monotreme / Egg-laying mammal)
Mamalia watagao mayai (Egg-laying mammals)

KinyamadegePlatypus
MhanganunguEchidna

Wednesday, May 25, 2011

Elki / Muusi (Moose)

Elki au Muusi (pia huitwa Kongoni wa Kaskazini) ni mnyama mkubwa wa Nusudunia ya Kaskazini anayefanana na kongoni mwenye pembe zenye umbo la matawi na manyoya mengi.


Kichwa kikubwaLarge head
Makwato ya shufwaEven-toed hooves
Miguu mirefu ya mbeleLong forelegs
Miguu mirefu ya nyumaLong hindlegs
Mkia mfupiShort tail
Nundu ya begaShoulder hump
Pembe zenye umbo la matawiRamified antlers
Pua inayoning'iniaDrooping muzzle
ShambweleleDewlap

Tuesday, May 24, 2011

Muundo wa Seli ya Mmea (The Structure of a Plant Cell)

Muundo wa seli ya mmea (The structure of a plant cell)

Chembe cha wangaStarch granule
Dutuvuo (Mitokondria)Mitochondrion
KiiniNucleus
Kiini kidogoNucleolus
Kitone cha asidi za shahamuLipid droplet
KitunduPore
Kiungo cha lamela za katiCompound middle lamella
KloroplastiChloroplast
Lamela ya katiMiddle lamella
LukoplastiLeucoplast
Nafasi kati ya seliIntercellular space
OganeliOrganelle
Oganeli ya GolgiGolgi apparatus
PeroksisomuPeroxisome
PlazmodesmaPlasmodesma
Retikulamu laini ya utegili wa ndaniSmooth endoplasmic reticulum
Retikulamu ya kukwaruza ya utegili wa ndaniRough endoplasmic reticulum
RibosomuRibosome
Seli ya mmeaPlant cell
Ukuta wa seliCell wall
Ukuta wa seli wa msingiPrimary sell wall
Utando wa kiiniNuclear envelope
Utando wa seliCell membrane
Utegili wa njeEctoplasma
Utegili wa seliCytoplasm
VakuoliVacuole

Maumbo ya Majani (Shapes of Leaves)



Maumbo ya Majani (Shapes of Leaves)

Umbo la figo Reniform
Umbo la kiganja Palmate
Umbo la klova Trifoliolate
Umbo la mkuki Lanceolate
Umbo la moyo Cordate
Umbo la mshale Hastate
Umbo la mstari Linear
Umbo la mviringo Orbiculate
Umbo la mwiko Spatulate
Umbo la ngao Peltate
Umbo la unyoya Pinnatifid
Umbo la unyoya shufwa Even-pinnate
Umbo la unyoya witiri Odd-pinnate
Umbo la yai Ovate 

Monday, May 23, 2011

Makali ya Majani (Leaf margins)

Makali ya majani (Leaf margins)

Umbo la ndeweLobate
Jani lenye makali mororoSmooth-edged leaf 
Jani lenye vinywele Ciliate leaf
Umbo la menoDentate
Umbo la meno ya mviringoCrenate
Umbo la menomenoDoubly dentate 

Friday, May 20, 2011

Sura za Mwezi (Phases of the Moon)

Sura ya mwezi (Moon phase)

Kufifia kwa mweziWaning gibbous
Kufifia kwa mwezi mwandamoWaning crescent
Kupevuka kwa mweziWaxing gibbous
Kupevuka kwa mwezi mwandamoWaxing crescent
Mwezi mchangaNew moon
Mwezi mpevuFull moon
Mwezi mwandamoCrescent moon
Mwezi mwandamo wa mwishoOld crescent
Mwezi ndani (Robo la mwisho)Last quarter
Mwezi nje (Robo la kwanza)First quarter
Nusu-mweziHalf moon

Wednesday, May 18, 2011

Hali ya Hewa (Weather)

Hali ya hewa (Weather)

DhorubaStorm
Hali ya hewa ni nzuri.The weather is nice.
Jua kali.It's sunny.
Kumetanda.It's overcast.
Kuna manyunyu.It's drizzling.
Kuna mawingu.It's cloudy.
Kuna mvua ya radi.There's a thunderstorm.
Kuna theluji inadondoka.It's snowing.
Kuna upepo.It's windy.
Mvua inanyesha.It's raining.
MweziMoon
TufaniTornado
Upinde wa mvuaRainbow

Tuesday, May 17, 2011

Aina za Mkate (Types of Bread)

Aina za mkate (Types of bread)
Mkate (Bread)

BageliBagel
Fimbo za mkateBreadsticks
Kinyunya ujeyaPhyllo dough
KrwasaniCroissant
Mikate midogoBread rolls
Mkate mgumu wa KiskandinaviScandinavian cracked bread
Mkate mgumu wa raiCracked rye bread
Mkate mweupeWhite bread
Mkate mweusi wa KirusiRussian pumpernickel
Mkate mweusi wa raiBlack rye bread
Mkate usiotiwa hamiraUnleavened bread
Mkate wa KieireIrish bread
Mkate wa KifaransaFrench bread (Baguette)
Mkate wa KigirikiGreek bread
Mkate wa KihindiIndian naan bread
Mkate wa KiingerezaEnglish bread
Mkate wa mhindiCornbread
Mkate wa mtindiButtermilk bread
Mkate wa nafaka zisizokobolewaMultigrain bread
Mkate wa raiRye bread
Mkate wa rai wa KidachiGerman rye bread
Mkate wa rai wa KideniDanish rye bread
Mkate-halaHallah bread
Mkate-pitaPita bread
SkonziBiscuit (Scone, Roll)
Tortila (Chapati ya mhindi)Tortilla

Aina za Viungo (Types of Spices)

Aina za viungo (Types of spices)
Kiungo (Spice)
mrihani; mrehani (basil)
majani ya mbei (bay leaves)
densi; dili (dill)
majorama (marjoram)
sage /seji/; aina ya mnanaa ulio majani yenye rangi ya kijani-kijivu (sage)
ufuta; uto; simsim (sesame)
basibasi (mace)
shamari (fennel)
kotimiri (parsley) 
taragoni (tarragon)
rosmeri; halwaridi (rosemary)
zaatari wa mwitu; majorama wa mwitu; majorama mtamu (oregano) 
zaatari wa kawaida; thaimu (thyme)


BizariCurry powder
DalasiniCinnamon
Haradali nyeupeWhite mustard
Haradali nyeusiBlack mustard
ManjanoTurmeric
IlikiCardamom
JiraCumin
KarafuuClove
KisibitiCaraway
KungumangaNutmeg
MasalaMasala
Mbegu za mpopiPoppy seeds
Pilipili iliyosagwaGround pepper
Pilipili kaliChili pepper
Pilipili mangaBlack pepper
Pilipili mbuziPaprika
Pilipili nyeupeWhite pepper
Pilipili ya JamaikaAllspice
Pilipili ya kijaniGreen pepper
Pilipili ya pinkiPink pepper
Pilipili zilizookwaDried chiles
Pilipili zilizopondwaCrushed chiles
Pilipili-halapenyoJalapeƱo pepper
ReteniJuniper berry
TangawiziGinger
UdahaCayenne pepper
Unga wa viungo vitanoFive spice powder
UwatuFenugreek
Viungo vya KikajuniCajun seasoning
ZafaraniSaffron

Matunda ya Tropiki (Tropical Fruits)

Tunda la tropiki (Tropical fruit)

CherimoyaCherimoya
DurianiDurian
EmbeMango
FeijoaFeijoa
FenesiJackfruit
Gakachika*Horned melon
GulabiLychee
Izu (Ndovi)Plantain
Jabotikaba (Zabibu ya Brazili)Jaboticaba
JohoPersimmon
Kinyomoro*Tamarillo
KiwiKiwi
KomamangaPomegranate
KunaziJujube
KuyuFig
LongyaniLongan
MangostanaMangosteen
NanasiPineapple
NdiziBanana
PapaiPapaya
PasheniPassion fruit
Pea la AsiaAsian pear
PeraGuava
PungatePrickly pear
SapodilaSapodilla
ShelisheliBreadfruit
ShokishokiRambutan
Tango tamuPepino
Tunda-nyotaStarfruit