Thursday, November 29, 2012

Watu-X #2 (The X-Men #2)

Watu-X dhidi ya Mtowekaji (The X-Men versus the Vanisher)
Hakuna awezaye kumshika Mtowekaji (No one can hold the Vanisher)

Mtowekaji, mwovu mwenye jeni-X aliye na uwezo wa kujihamisha kutoka mahali pamoja kwenda pengine papo hapo, aliibia benki ya taifa na kusaliti Pembetano (makao makuu ya jeshi la Marekani). Watu-X wampinga yeye alipokuwa akiibia ramani za ulinzi wa serikali. Hata hivyo, hawakuweza kupigana na mhalifu huyo, kwa sababu akajihamisha nje ya masafa. Profesa X aliwaokoa kwa kumzuia Mtowekaji asitumie uwezo wake wa pekee kwa kutumia akili yake tu.

The Vanisher, an evil mutant with the power of teleportation (to transport himself from one place to another in an instant), robbed the national bank and blackmailed the Pentagon (the main headquarters of the American army). The X-Men face him, as he was stealing the government's defense plans. However, they were unable to fight this villain, because he teleported out of range. Professor X saved them by preventing the Vanisher from using his mutant powers with only his mind.


Watu-X #1 (The X-Men #1)

Watu-X dhidi ya Magneto (The X-Men versus Magneto)

Katika shule maalum ya binafsi katika wilaya ya Westchester, Profesa Charles Xavier afundisha jamii maalum ya vijana wanne wa kiume, kila mtu mwenye uwezo utokanao na jeni-X. Baada ya kuwaangalia kwa makini wakifanya mazoezi yao, Xavier aliwaambia wanafunzi wake: Malaika, Mtu wa Barafu, Hayawani na Saiklopsi, kwamba mwanafunzi wa tano atafika leo. 

In a special private school in Westchester county, Professor Charles Xavier teaches a special class of young men, each one with a mutant power. After carefully watching them do their exercises, Xavier told his students: Angel, Iceman, Beast and Cyclops, that the fifth student will arrive today.

Kwa furaha yao, vijana wanne waona kwamba mwanafunzi mpya ni msichana mrembo sana mwenye nywele nyekundu. Jina lake ni Jean Grey na akakaribishwa vizuri kwenye jumba lao la ghorofa. Vijana wanne wakashangaa kwa urembo wake. Jean alipowaonyesha uwezo wake wa kusongeza vifaa kwa akili yake (uwezo unaojulikana kama telekinesisi), Profesa X, aliye pia na nguvu za pekee mwenyewe, alimwambia yeye kuhusu nia halisi ya shule yake. 

To their delight, the four young men see that the new student is a very beautiful redheaded girl. Her name is Jean Grey and was then welcomed into their mansion. The four young men were amazed by her beauty. After Jean showed them her power to move objects with her mind (a power known as telekinesis), Professor X, who also has special powers himself, told her about the real purpose of his school. 

Kwanza, shule hiyo ni mahali pa usalama kwa watu wote wenye jeni-X, kwa sababu ubinadamu bado hauko tayari kukubali watu wenye uwezo wa ajabu kama wao; hata hivyo, shule hiyo pia hufanya kazi kama uwanja wa mazoezi ili kuwatayarisha wanafunzi wake wanaojulikana kama Watu-X kwa vita vijavyo dhidi ya waovu wenye jeni-X wanaojiangalia kuwa na cheo cha juu zaidi kuliko cha binadamu wa kawaida na wanataka kuwatawala. 

First of all, the school is a safe haven for all mutants, because humanity is not yet ready to accept people with superpowers like theirs; however, this school also serves as a training field in order to prepare his students who are known as the X-Men for future battles against evil mutants who view themselves as having a higher rank than that of regular humans and want to rule them.

Siku inayofuata mwenye jeni-X mmoja kama hao kwa jina la Magneto alikishambulia kituo cha makombora “Rasi ya Ngome”, na alikijitwalia. Xavier akawatuma Watu-X wamsimamishe. Kwa sababu ya ngao za kisumaku zilizoumbwa na Magneto, jeshi halikuweza kuingia ndani kituo. Magneto hakuweko tayari kupigana na watu wengine wenye jeni-X, kwa hivyo vijana watano wa Watu-X walifaulu na wakashinda mashambulio yote ya Magneto kwa kazi ya kikoa. Ingawa Magneto alitoroka, jeshi liliwashukuru Watu-X. Mwishowe Profesa X aliwahongeza wanafunzi wake kwa ushindi wao wa kwanza.

The following day a mutant like that by the name of Magneto attacked the "Cape Citadel" missile base, and he seized it for himself. Xavier sent the X-Men to stop him. Because of the magnetic shield created by Magneto, the army was unable to get into the base. Magneto was not ready to fight other mutants, so the five young X-Men succeeded and defeated all of Magneto's attacks with teamwork. Although Magneto escaped, the army thanked the X-Men. In the end, Professor X congratulated his students on their first victory.

Saturday, November 10, 2012

Mshenzi (Feral)

 
Mshenzi (Feral)

Mshenzi ni mhusika wa bunilizi anayetokea katika Ulimwengu wa Marvel. Yeye amekuwa shujaa na pia mhalifu na pia anajulikana kama mwanachama wa Nguvu-X. Mshenzi alipojaribu kutoroka kutoka mtawala dhalimu wa Morloki aitwaye Maskhara, akaokolewa na Kebo kutoka kwa Maskhara, na akajiunga na timu ya Kebo ili kuwa mwanachama wa Nguvu-X .  Yeye ni mpiganaji mkatili kutokana na matayarisho yake pamoja na Kebo. Yeye ana mutesheni ya paka iliyompa kucha na chonge kali, hisia kali za ajabu, uwezo wa kuona kwenye giza, nguvu iliyozidishwa, uwezo wa kujiponya haraka, mkia na manyoya ya machungwa yanayofunika mwili wake.
 
Feral is a fictional character appearing in the Marvel Universe. She has been both a hero and a villain and is also known as a member of X-Force. When Feral tried to escape from the tyrannical ruler of Morlocks named Masque, she was saved by Cable and then joined Cable's team in order to become a member of X-Force. She is a fierce fighter due to her training with Cable. She has a feline mutation that gave her sharp claws and fangs, superhumanly acute senses, the ability to see in the dark, enhanced strength, the ability to heal quickly, a tail and orange fur covering her body.

Friday, November 9, 2012

Baharia Zebaki (Sailor Mercury)


Baharia Zebaki (Sailor Mercury)

Baharia Zebaki alikuwa Skauti-Baharia wa kwanza aliyejiunga na Baharia Mwezi katika mapigano dhidi ya Ufalme wa Giza. Yeye huwa mfanya-mikakati wa Baharia-Askari wa Ndani na hutumia tarakilishi ya mikono kama skana na kichanganua-data. Rangi anayoipenda zaidi ni samawati. Hupenda kusoma, kucheza sataranji na kuogelea. Vyakula anavyovipenda zaidi ni sandwichi na anmitsu (jeli iliyotengenezwa kwa mwani mwekundu na maharagwe ya azuki). Chakula asichokipenda ni bangala mkia-manjano.
Sailor Mercury was the first Sailor Scout to join Sailor Moon in the fight against the Dark Kingdom. She is the strategist of the Inner Sailor Soldiers and uses a hand-held computer as a scanner and data analyzer. Her favorite color is sky-blue. She likes to read, play chess and swim. Her favorite foods are sandwiches and anmitsu (a jelly made from red algae and azuki beans). Her least favorite food is yellowtail.

Mashambulio

Viputo vya Zebaki (Mercury Bubbles)

Shambulio lake la kwanza linaitwa “Viputo vya Zebaki!” (kwa Kiingereza: Mercury Bubbles Blast!; Kijapani: Bubble Spray!). Shambulio hili hutengeneza ukungu ambao humpofusha adui.
Her first attack is called "Mercury Bubbles!" (in English: Mercury Bubbles Blast!; Japanese: Bubble Spray!). This attack produces fog that blinds the enemy.

Sunday, November 4, 2012

Wolverini (Wolverine)

Wolverini (Wolverine)

Wolverini (jina halisi: James Howlett; pia anajulikana kama Logan) ni mhusika wa bunilizi, shujaa wa ajabu anayetokea katika vitabu vya komiki vilivyochapishwa na Marvel Comics. Wolverini ni mwenye jeni-X ambaye humiliki hisia kali za kinyama, nguvu ya kimaumbile iliyozidishwa, kucha tatu za mfupa, kipengele cha kujiponya ambacho humwezesha kupona haraka zaidi kuliko binadamu wa kawaida. Kipengele chake cha kujiponya chenye nguvu kiliiwezesha shirika iitwayo Silaha-X kugundisha kiunzi chake cha mifupa kwa adamantiamu, aloi ya metali isiyoharibika, bila kumwua. Mara nyingi yeye huchorwa kama mwanachama wa Watu-X, Kundi Alfa au baadaye wa Walipiza-kisasi.

Wolverine (real name: James Howlett; also known as Logan) is a fictional character, a superhero appearing in comic books published by Marvel Comics. Wolverine is a mutant who possess keen animalistic senses, enhanced physical power, three bone claws, a healing factor which enables him to recover faster than an average human. His powerful healing factor enabled the organization called Weapon-X to bond to his skeleton adamantium, an indestructible metal alloy, without killing him. He often is depicted as a member of the X-Men, Alpha Flight or later of the Avengers.

kumiliki = to possess
mwenye jeni-X = mutant
hisia kali = keen senses
iliyozidishwa = enhanced
ya kimaumbile = physical
kucha za mfupa = bone claws
kipengele cha kujiponya = healing factor
kipengele cha kuongoa uponyaji = regenerative healing factor
yenye nguvu = powerful
kuwezesha = to enable
kupona = to recover
adamanti = adamantium
isiyoharibika = indestructible

Saiklopsi (Cyclops)

Saiklopsi (Cyclops)

Saiklopsi (Jina halisi: Scott Summers) ni mhusika wa bunilizi ambaye hutokea katika vitabu vya komiki vilivyochapishwa na Marvel Comics. Mara nyingi huwa kiongozi mkuu wa Watu-X. Yeye huvaa miwani yenye kioo kimoja kilichotengezwa kwa kwatsi ya rubi. Ndiyo maana alipewa jina la siri la “Saiklopsi”. Akiwa mwenye jeni-X, Saiklopsi ana uwezo wa kuvurumisha vilipuzi vya nishati kutoka kwa macho yake vilivyoelezwa kama “vilipuzi vya macho”. Vilipuzi hivi vinaonekana kama nuru nyekundu (yaani mnururisho wa kisumaku-umeme katika masafa ya mawimbi mekundu); hata hivyo, havitoi joto. Vilipuzi hivi vina nguvu sana na huweza kutumika kupasua sahani za feleji na kuponda miamba kuwa vumbi.

Cyclops (Real name: Scott Summers) is a fictional character who appears in comic books published by Marvel Comics. He is often the main leader of the X-Men. He wears glasses with one lens made from ruby quartz. This is why he was given the code name of "Cyclops". Being a mutant, Cyclops has the ability to shoot energy blasts from his eyes described as "optic blasts". These blasts resemble red light (i.e. electromagnetic radiation in red wavelengths); however, they do not give off heat. These blasts are very powerful and can be used to rupture steel plates and crush rocks into dust.

kuchapishwa = to be published
kiongozi = leader
-kuu = main
miwani = glasses
kutengezwa kwa = to be made of
kwatsi ya rubi = ruby quartz
kilipuzi cha jicho = optic blast
nuru = light
mnururisho = radiation
-a kisumaku-umeme = electromagnetic
kutoa = to give off/out
joto = heat
kupasua = to rupture
feleji = steel
kuponda kuwa vumbi = to pulverize