Sunday, November 4, 2012

Saiklopsi (Cyclops)

Saiklopsi (Cyclops)

Saiklopsi (Jina halisi: Scott Summers) ni mhusika wa bunilizi ambaye hutokea katika vitabu vya komiki vilivyochapishwa na Marvel Comics. Mara nyingi huwa kiongozi mkuu wa Watu-X. Yeye huvaa miwani yenye kioo kimoja kilichotengezwa kwa kwatsi ya rubi. Ndiyo maana alipewa jina la siri la “Saiklopsi”. Akiwa mwenye jeni-X, Saiklopsi ana uwezo wa kuvurumisha vilipuzi vya nishati kutoka kwa macho yake vilivyoelezwa kama “vilipuzi vya macho”. Vilipuzi hivi vinaonekana kama nuru nyekundu (yaani mnururisho wa kisumaku-umeme katika masafa ya mawimbi mekundu); hata hivyo, havitoi joto. Vilipuzi hivi vina nguvu sana na huweza kutumika kupasua sahani za feleji na kuponda miamba kuwa vumbi.

Cyclops (Real name: Scott Summers) is a fictional character who appears in comic books published by Marvel Comics. He is often the main leader of the X-Men. He wears glasses with one lens made from ruby quartz. This is why he was given the code name of "Cyclops". Being a mutant, Cyclops has the ability to shoot energy blasts from his eyes described as "optic blasts". These blasts resemble red light (i.e. electromagnetic radiation in red wavelengths); however, they do not give off heat. These blasts are very powerful and can be used to rupture steel plates and crush rocks into dust.

kuchapishwa = to be published
kiongozi = leader
-kuu = main
miwani = glasses
kutengezwa kwa = to be made of
kwatsi ya rubi = ruby quartz
kilipuzi cha jicho = optic blast
nuru = light
mnururisho = radiation
-a kisumaku-umeme = electromagnetic
kutoa = to give off/out
joto = heat
kupasua = to rupture
feleji = steel
kuponda kuwa vumbi = to pulverize

No comments:

Post a Comment