Thursday, November 29, 2012

Watu-X #1 (The X-Men #1)

Watu-X dhidi ya Magneto (The X-Men versus Magneto)

Katika shule maalum ya binafsi katika wilaya ya Westchester, Profesa Charles Xavier afundisha jamii maalum ya vijana wanne wa kiume, kila mtu mwenye uwezo utokanao na jeni-X. Baada ya kuwaangalia kwa makini wakifanya mazoezi yao, Xavier aliwaambia wanafunzi wake: Malaika, Mtu wa Barafu, Hayawani na Saiklopsi, kwamba mwanafunzi wa tano atafika leo. 

In a special private school in Westchester county, Professor Charles Xavier teaches a special class of young men, each one with a mutant power. After carefully watching them do their exercises, Xavier told his students: Angel, Iceman, Beast and Cyclops, that the fifth student will arrive today.

Kwa furaha yao, vijana wanne waona kwamba mwanafunzi mpya ni msichana mrembo sana mwenye nywele nyekundu. Jina lake ni Jean Grey na akakaribishwa vizuri kwenye jumba lao la ghorofa. Vijana wanne wakashangaa kwa urembo wake. Jean alipowaonyesha uwezo wake wa kusongeza vifaa kwa akili yake (uwezo unaojulikana kama telekinesisi), Profesa X, aliye pia na nguvu za pekee mwenyewe, alimwambia yeye kuhusu nia halisi ya shule yake. 

To their delight, the four young men see that the new student is a very beautiful redheaded girl. Her name is Jean Grey and was then welcomed into their mansion. The four young men were amazed by her beauty. After Jean showed them her power to move objects with her mind (a power known as telekinesis), Professor X, who also has special powers himself, told her about the real purpose of his school. 

Kwanza, shule hiyo ni mahali pa usalama kwa watu wote wenye jeni-X, kwa sababu ubinadamu bado hauko tayari kukubali watu wenye uwezo wa ajabu kama wao; hata hivyo, shule hiyo pia hufanya kazi kama uwanja wa mazoezi ili kuwatayarisha wanafunzi wake wanaojulikana kama Watu-X kwa vita vijavyo dhidi ya waovu wenye jeni-X wanaojiangalia kuwa na cheo cha juu zaidi kuliko cha binadamu wa kawaida na wanataka kuwatawala. 

First of all, the school is a safe haven for all mutants, because humanity is not yet ready to accept people with superpowers like theirs; however, this school also serves as a training field in order to prepare his students who are known as the X-Men for future battles against evil mutants who view themselves as having a higher rank than that of regular humans and want to rule them.

Siku inayofuata mwenye jeni-X mmoja kama hao kwa jina la Magneto alikishambulia kituo cha makombora “Rasi ya Ngome”, na alikijitwalia. Xavier akawatuma Watu-X wamsimamishe. Kwa sababu ya ngao za kisumaku zilizoumbwa na Magneto, jeshi halikuweza kuingia ndani kituo. Magneto hakuweko tayari kupigana na watu wengine wenye jeni-X, kwa hivyo vijana watano wa Watu-X walifaulu na wakashinda mashambulio yote ya Magneto kwa kazi ya kikoa. Ingawa Magneto alitoroka, jeshi liliwashukuru Watu-X. Mwishowe Profesa X aliwahongeza wanafunzi wake kwa ushindi wao wa kwanza.

The following day a mutant like that by the name of Magneto attacked the "Cape Citadel" missile base, and he seized it for himself. Xavier sent the X-Men to stop him. Because of the magnetic shield created by Magneto, the army was unable to get into the base. Magneto was not ready to fight other mutants, so the five young X-Men succeeded and defeated all of Magneto's attacks with teamwork. Although Magneto escaped, the army thanked the X-Men. In the end, Professor X congratulated his students on their first victory.

No comments:

Post a Comment