Sunday, November 4, 2012

Wolverini (Wolverine)

Wolverini (Wolverine)

Wolverini (jina halisi: James Howlett; pia anajulikana kama Logan) ni mhusika wa bunilizi, shujaa wa ajabu anayetokea katika vitabu vya komiki vilivyochapishwa na Marvel Comics. Wolverini ni mwenye jeni-X ambaye humiliki hisia kali za kinyama, nguvu ya kimaumbile iliyozidishwa, kucha tatu za mfupa, kipengele cha kujiponya ambacho humwezesha kupona haraka zaidi kuliko binadamu wa kawaida. Kipengele chake cha kujiponya chenye nguvu kiliiwezesha shirika iitwayo Silaha-X kugundisha kiunzi chake cha mifupa kwa adamantiamu, aloi ya metali isiyoharibika, bila kumwua. Mara nyingi yeye huchorwa kama mwanachama wa Watu-X, Kundi Alfa au baadaye wa Walipiza-kisasi.

Wolverine (real name: James Howlett; also known as Logan) is a fictional character, a superhero appearing in comic books published by Marvel Comics. Wolverine is a mutant who possess keen animalistic senses, enhanced physical power, three bone claws, a healing factor which enables him to recover faster than an average human. His powerful healing factor enabled the organization called Weapon-X to bond to his skeleton adamantium, an indestructible metal alloy, without killing him. He often is depicted as a member of the X-Men, Alpha Flight or later of the Avengers.

kumiliki = to possess
mwenye jeni-X = mutant
hisia kali = keen senses
iliyozidishwa = enhanced
ya kimaumbile = physical
kucha za mfupa = bone claws
kipengele cha kujiponya = healing factor
kipengele cha kuongoa uponyaji = regenerative healing factor
yenye nguvu = powerful
kuwezesha = to enable
kupona = to recover
adamanti = adamantium
isiyoharibika = indestructible

No comments:

Post a Comment