Friday, November 9, 2012

Baharia Zebaki (Sailor Mercury)


Baharia Zebaki (Sailor Mercury)

Baharia Zebaki alikuwa Skauti-Baharia wa kwanza aliyejiunga na Baharia Mwezi katika mapigano dhidi ya Ufalme wa Giza. Yeye huwa mfanya-mikakati wa Baharia-Askari wa Ndani na hutumia tarakilishi ya mikono kama skana na kichanganua-data. Rangi anayoipenda zaidi ni samawati. Hupenda kusoma, kucheza sataranji na kuogelea. Vyakula anavyovipenda zaidi ni sandwichi na anmitsu (jeli iliyotengenezwa kwa mwani mwekundu na maharagwe ya azuki). Chakula asichokipenda ni bangala mkia-manjano.
Sailor Mercury was the first Sailor Scout to join Sailor Moon in the fight against the Dark Kingdom. She is the strategist of the Inner Sailor Soldiers and uses a hand-held computer as a scanner and data analyzer. Her favorite color is sky-blue. She likes to read, play chess and swim. Her favorite foods are sandwiches and anmitsu (a jelly made from red algae and azuki beans). Her least favorite food is yellowtail.

Mashambulio

Viputo vya Zebaki (Mercury Bubbles)

Shambulio lake la kwanza linaitwa “Viputo vya Zebaki!” (kwa Kiingereza: Mercury Bubbles Blast!; Kijapani: Bubble Spray!). Shambulio hili hutengeneza ukungu ambao humpofusha adui.
Her first attack is called "Mercury Bubbles!" (in English: Mercury Bubbles Blast!; Japanese: Bubble Spray!). This attack produces fog that blinds the enemy.

No comments:

Post a Comment