Monday, August 25, 2014

Baharia Zohali (Sailor Saturn)

Baharia Zohali (Sailor Saturn)
Baharia Zohali anatambulishwa mara ya kwanza anapokuwa rafiki ya Chibi-Usa. Alikuwa mnyamavu asiyeonyesha hisia, mwenye kukomaa upesi akili na mdani, na kusema machache, huwa hapendwi sana na wanafunzi wenzake kwa sababu ya nguvu zake na utekaji wake wa kioja pamoja na mabadiliko yake mengi ya nafsi kutoka kuwa mwenyeji wa Bibi Tisa (kiumbe kiovu kilichoishi ndani yake toka akiwa na miaka 5). 

Sailor Saturn is first introduced when she becomes friends with Chibi-Usa. She was quiet, expressionless, precocious and an introvert, and to say the least, not very popular with her classmates because of her powers and her strange seizures as well as multiple personality changes for being the host of Mistress Nine (the evil entity that lived in her since the age of 5).  

Mabadiliko ya Bibi Tisa (Transformation of Mistress 9)
Baada ya maabara ya babake kulipuka na kuua mamake Hotaru, babake alimwokoa kwa kufanya mwili wake saibentiki na kufanya mkataba na Farao 90.  Kwa kubadilishana, babake alipoteza ubinadamu wake na kuwa mtu mwovu.

After her father’s laboratory exploded, killing Hotaru's mother and critically injuring Hotaru, her father rescued her by making her body cybernetic and made a deal with Pharaoh 90. In exchange, her father lost his humanity and became malevolent. 

Kwa Nguvu ya Sayari ya Zohali (Saturn Planet Power)
Kama askari, Baharia Zohali alimiliki nguvu za ajabu sana za kuharibu, hivi kwamba uamusho wake uliogopwa na Skauti wa Nje; hata hivyo, kwa kutumia nguvu zake kikamilifu ungesababisha kifo chake.

As a Sailor Scout, Sailor Saturn possessed such awesome destructive power that her awakening was feared by the Outer Scouts; however, using her powers to their full extent would bring about her death. 

Ukuta wa Kimya (Silent Wall)
Yeye hutoa nguvu zake zote kutoka mkukishoka wa kunyamaza ambayo inaweza kuunda kizuizi cha kujikinga yeye na wengine dhidi ya mashambulizi ya adui.

She derives all of her powers from her silence glaive that can create a protective barrier around herself and others against enemy attacks. 

Mkukishoka wa Kunyamaza (Silence Glaive)
Shambulizi lake la nguvu zaidi husababisha ukungu mzito ambayo kwanza huwachanganya adui wake wakati ambapo anajitayarisha kwa shambulizi ya ghafla na mradi ncha ya mkukishoka wake inateremshwa hadi ardhini mlipuko wa miali ya nishati ya zambarau humzunguka na kuangamiza eneo linalomzunguka.

Her most power attack produces a thick fog to first disorient her enemy, as she prepares for a surprise attack and once the tip of her glaive is lowered to the ground a radial explosion of purple energy surrounds her and decimates the area around her.

No comments:

Post a Comment