Monday, August 25, 2014

Pepo Anayerudi (Returning Spirit)


Pepo anayerudi (A returning spirit)
Pepo anayerudi (pia anayejulikana kama revenant kwa Kifaransa na Wiedergänger kwa Kijerumani) ni pepo anayeonekana wa mtu aliyekufa ambaye alikuwa mwovu, ovyo au kafiri ambaye anaaminika kurudi kutoka kwenye kaburi na kuwahangaisha wanaoishi; ingawaje hekaya na hadithi za baadaye zinawasawiri revenanti wakirudi hasa kwa sababu maalum (k.m. kulipiza kisasi dhidi ya muuaji wa marehemu). Katika rekodi nyingi za enzi ya kati, wao hurudi kuwahangaisha familia na majirani wanaoishi na huweza hata kueneza magonjwa  kati ya wanaoishi.

A returning spirit (also known as revenant in French and Wiedergänger in German) is the visible spirit of a dead person who was wicked, vain or a non-believer, that is believed to return from the grave to terrorize the living; though later legend and folklore depict revenants as returning for a specific purpose (e.g. revenge against the deceased’s killer). In most medieval accounts they return to harass their surviving families and neighbours, and may spread disease among the living.

Wiedergänger
Tafsiri la Kijerumani la pepo anayerudi ni maiti aliyepewa uhai, kama kizuu, ambaye amerudi ulimwengu wa wanaoishi. Wao husababisha matatizo na kushtua watu wanaoishi. Wao huishi kulipiza kisasi kwa dhuluma fulani walizopitia walipokuwa hai, au kwa sababu roho yao haiko tayari kuachiliwa kutokana na hali ya maisha yao ya hapo awali.

The German version of a returning spirit is an animated corpse, like a zombie, that has returned to the world of the living. They usually cause problems and frighten living people. They exist either to avenge some injustice they experienced while alive, or because their soul is not ready to be released, as a consequence of their former way of life.

No comments:

Post a Comment