Monday, August 25, 2014

Baharia Pluto (Sailor Pluto)

Baharia Pluto (Sailor Pluto)
Baharia Pluto ni mwanafizikia na aghalabu huonekana na wenzake kama aliyetengwe na jamii au mpweke; hata hivyo, yeye kwa kawaida huonyesha wema na mapenzi kwa Chibi-Usa (Baharia Mwezi Mdogo). Baada ya kuzaliwa tena, yeye huwa na urafiki zaidi, lakini bado si mwenye mchemuko. Yeye hufanya kazi kama mlinzi wa lango kuu la wakati na anga. Wakati mwingine, yeye huonyesha vitendo vya kuwa na maarifa yote na hudhaniwa kuwa anajua vitendo vyote vya wenzake wake wakati ambapo anapowatazama kutoka kiungo cha wakati na anga. 

Sailor Pluto is a physicist and tends to be seen by her teammates as an outcast or loner; however, she does consistently display warmth and affection for Chibi-Usa (Sailor Mini Moon). After she is reincarnated, she becomes friendlier, but is still not very emotional. She acts as the guardian of the portal of time and space. At times, she displays acts of omniscience and is presumed to be aware of all acts of her teammates as she watches from the nexus of time and space.

Tufe ya Ganeti (The Garnet Orb)
Juu ya mkongojo-ufunguo wake hukaa tufe ya ganeti (hirizi yenye nguvu ambayo humruhusu kufungua mlango wa anga na wakati). 

Atop her keystaff sits the garnet orb (a powerful talisman that allows her to open the space-time door).

Yowe la Wafu (Dead Scream)
Shambulizi analotumia zaidi linaitwa "Yowe la Wafu". Hata hivyo, yeye ndiye skauti-baharia wa pekee ambaye huwa hapigi unyende amri yake ya shambulizi.

Her most used attack is called "Dead Scream". However, she is the only sailor scout who does not scream her attack command.

Kituo cha Wakati (Time Stop)
Kwa nguvu ya hirizi hii, yeye pia anaweza kusimamisha wakati; hata hivyo, hii ni nguvu iliyokatazwa ambayo ilisababisha kifo chake.

With this talisman, she can also stop time; however, this is a forbidden power, which resulted in her death. 

No comments:

Post a Comment