Tuesday, January 15, 2013

Watu-X #4 (The X-Men #4)

Undugu wa Vioja Viovu (The Brotherhood of Evil Mutants) 

Undugu wa Vioja Viovu utambulishwa. Magneto alileta pamoja timu inayotungwa kwa Jura mchupaji, mfanya-mauzauza Mwanzilishi Mwamba, Zebaki - mkimbiaji wa kasi ya juu na dada yake Mchawi Mwekundu. Undugu ulitwaa taifa dogo katika Amerika Kusini baada ya saa chache tu, kwa hivyo, Xavier na Watu-X walikwenda huko na kupigana na kundi hilo. Hata hivyo, walikuwa na matata, kwa sababu hawakuzoea nguvu za wapinzani wao. Mwishowe Undugu ulifukuzwa, lakini uliacha mabomu machache nyuma. Halafu, Xavier akajitupa mbele ya mlipuko, na kwa hivyo, akapotea telepathia yake. Chombo cha pili kilikuwa bomu la nyuklia lililowekwa kuangamiza nchi nzima, lakini Zebaki alilichangua kabla ya kuondoka. Kwa kweli, Zebaki na Mchawi Mwekundu siyo waovu, bali hutumikia Magneto kwa ajili ya deni. Magneto alimwokoa Mchawi Mwekundu kutoka kwa kundi la watu wenye hasira baada ya yeye kuteketeza kihenge katika kijiji chake cha kuzaliwa.

The Brotherhood of Evil Mutants is introduced. Magneto brought together a team consisting of the hopping Toad, the illusionist Mastermind, Quicksilver the high-speed runner and his sister the Scarlet Witch. The Brotherhood took over a small nation in South America after only a few hours, therefore, Xavier and the X-Men went there to fight the group. However, they had problems, because they were not familiar with their opponents' powers. In the end, the Brotherhood was driven off, but left some bombs behind. Then, Xavier threw himself in front of the explosion, and thus, lost his telepathy. The second device was a nuclear bomb that was set to destroy the whole country, but Quicksilver disarmed it before leaving. Actually, Quicksilver and the Scarlet Witch are not evil, but serve Magneto on account of a debt. Magneto rescued Scarlet Witch from an angry mob after she burned down a barn in her native village.

No comments:

Post a Comment