Saturday, January 5, 2013

Biarusi wa Frankenstein (Bride of Frankenstein)

Biarusi wa Frankenstein (Bride / Brides of Frankenstein) 

Usiku mmoja wenye giza na dhoruba, Viktori aliumba mwenzi wa kike wa dubwana wake. Biarusi wa Frankeinstein alipata uhai wakati radi ilipopiga kishada ambayo ilipeleka umeme kupitia maiti ya kike iliyojengwa kwa mtindo sawa na ya mwenzi wake wa kiume. Biarusi anavalia gauni lililofungwa kwa bendeji na mtindo wa nywele kama pia ulio na mistari miwili myeupe ya radi kwenye nywele inayoanzia kwenye mapanja ya pande zote mbili za kichwa chake.

On a dark and stormy night, Victor created a female counterpart of his monster. The bride of Frankenstein was brought to life when lightning struck a kite which sent electricity through a female corpse built by the same method of her male counterpart. The bride wears a dress wrapped with bandages and a conical hairdo with two white lightning streaks in her hair starting from the temples on both sides of her head.

yenye giza = dark
yenye dhoruba = stormy
radi = lightning
kupiga = to strike
kishada = kite
kupeleka = to send
kujengwa = to be built
gauni = dress
iliyofungwa kwa = wrapped with
mtindo wa nywele = hairdo
pia = cone
mstari = line / streak
panja = temple (of head) 

No comments:

Post a Comment