Friday, January 4, 2013

Dhampiri (Dhampirs)

Dhampiri (Dhampir / Dhampirs) 
Dhampiri, au nusu-mnyonyadamu, katika hadithi za Balkani ni mtoto wa mnyonyadamu na binadamu. Nguvu za dhampiri ni sawa na zile za wanyonyadamu, lakini bila udhaifu wa kawaida. Dhampiri wengi hudharau upande wa giza wa urithi wao na huwa wawinda-wanyonyadamu, na wanadhaniwa kuwa stadi katika kugundua na kuua wanyonyadamu. Neno la dhampiri linaaminika kutokana na neno la Kialbania dham “meno” na pirë “kunywa”. Wanyonyadamu huwa na ashiki kubwa kwa wanawake, hivyo aliyegeuzwa kuwa mnyonyadamu hivi karibuni atarudi kujamiiana na mkewe au mwanamke aliyempendeza katika maisha yake, na wanyonyadamu Wabulgaria hasa huwa na tamaa ya kubikiri mabikira.

A dhampir, or half-vampire, in Balkan tales is the child of a vampire and a human. Dhampir powers are similar to those of vampires, but without the usual weaknesses. Many dhampirs despise the dark side of their heritage and become vampire hunters, and are believed to be skilled in detecting and killing vampires. The word dhampir is believed to derive from the Albanian word dham "teeth" and pirë "to drink". Vampires have a desire for women, so one who was changed into a vampire recently will return to have intercourse with his wife or the woman who was attractive to him in his life, and Bulgarian vampires especially passion to deflower virgins. 

mnyonyadamu = vampire
nusu-mnyonyadamu = half-vampire
urithi = heritage
mwinda-wanyonyadamu = vampire hunter
Kialbania = Albanian (adj.)
hivi karibuni = recently
kujamiiana na = to mate with / to have intercourse with
mkewe = his wife
maisha = life(-time)
Mbulgaria = Bulgarian (person)
Wabulgaria = Bulgarians (people)
kubikiri = to deflower (a virgin)
bikira = virgin

No comments:

Post a Comment