Sunday, March 4, 2018

Watu-X #9 (The X-Men #9)

Walipiza-Kisasi na Lusiferi (The Avengers and Lucifer)

Watu-X wamfuata Profesa X kwenda Ulaya ambako anamtafuta Lusiferi, adui wa zamani, aliyemlemaza miaka mingi iliyopita. Lusiferi amfunulia Profesa, kwamba ametumia miaka kumi kuunda bomu la joto lililounganishwa na mpigo wa moyo wake. Kama angeuliwa au angedhuriwa kwa namna yoyote, bomu lingelipuka na kusababisha madhara ya ulimwenguni pote. Kwa nasibu, Walipiza-Kisasi pia wafika kuchunguza mitetemo ya kigeni yanayotoka katika bomu la Lusiferi ambayo yaligunduliwa na nyundo ya Thor, iitwayo Mjølnir. Hata hivyo, Watu-X walazimishwa kupigana nao ili kuwazuia wasimshambulie adui yao. Kwa bahati nzuri, wakati ambapo Lusiferi anakengeushwa na mapigano kati ya timu mbili za mashujaa, Profesa X kwa telepathia alimpiga adui yake mpaka akazimia bila kubadili mpigo wa moyo wake. Baada ya kueleza yote kwa Walipiza-Kisasi, Watu-X waharakisha kwenda ficho la Lusiferi, ambamo Saiklopsi na Profesa wafaulu kutegua bomu hilo. Na hatimaye, Profesa X amwamsha Lusiferi, na Watu-X waamua kumwacha nyuma pangoni mwake na halafu warudi jumba lao.

The X-Men follow Professor X to Europe where he is tracking down Lucifer, an old enemy, who is crippled him years ago. Lucifer reveals to the Professor, that he has spent the last 10 years building a thermal detonator that is attached to his heartbeat. If he is killed or harmed in any way, it will blow up, causing worldwide damage. Coincidentally, the Avengers also arrive to investigate the strange vibrations emanating from Lucifer's bomb that were detected by Thor's hammer, Mjølnir. However, the X-Men are forced to fight them in order to prevent them from attacking their mutual enemy. Luckily, while Lucifer is distracted by the battle between the two teams of heroes, Professor X telepathically knocks his foe unconscious without changing his heartbeat. After explaining everything to the Avengers, the X-Men hurry to Lucifer's hidden cave, where Cyclops and the Professor manage to diffuse the bomb. Professor X ultimately wakes Lucifer up, and the X-Men ultimately decide to leave him behind in his cave and then return to the mansion.

No comments:

Post a Comment