Thursday, March 8, 2018

Watu-X #11 (The X-Men #11)

Mgeni (The Stranger)

Baada ya kugundua saini ya nishati yenye nguvu sana, Undugu na Watu-X pia wajaribu kuandikisha mtu mwingine mwenye jeni-X. Undugu wawasiliana naye kwanza, kwa hiyo Magneto na Bwana Akili wajaribu kumvutia mgeni huyo kwa uwezo wao. Mwishowe, wamkasirisha mwanachama wao mpya mtarajiwa, ambaye kisha ageuza Bwana Akili kuwa jiwe. Watu-X wafikapo, Mgeni ateka nyara Magneto na Jura pia na kutokomea mbali. Sasa kwa kuwa Magneto ametoweka, Zebaki na Mchawi Mwekundu waamini kwamba wamelipa deni lao kwa Magneto, kwa hiyo waamua kurudi katika nchi yao ya kuzaliwa barani Ulaya. 

Karibu na hapo, Watu-X wamfikia yule mtu mpya mwenye jeni-X ambaye ajifunua kuwa kiumbe kutoka anga la nje aitwaye Mgeni. Watu wa spishi yake wanapendezwa na mabadiliko jeni, na hivyo ndivyo Mgeni achungua Magneto na Jura wawe vielelezo vyake vipya, kwa kuwa walisisitiza kuungana naye tangu mwanzoni kabisa. Watu-X waweza kusimama na kutazama tu huku maadui zao wanapopaa angani. Tena nyumbani, Cerebro yatambua kwamba mtu mwingine mwenye nguvu nyingi yuko karibu sana.

After detecting a very powerful energy signature, both the Brotherhood and the X-Men attempt to recruit another mutant. The Brotherhood makes first contact, so Magneto and Mastermind try to impress this stranger with their abilities. They end up annoying their potential recruit, who then changes Mastermind to stone. As the X-Men arrive, the Stranger kidnaps both Magneto and Toad and vanish into thin air. Now that Magneto is gone, Quicksilver and the Scarlet Witch believe that they have worked off their debt to Magneto, so they decide to return to their native land in Europe.

Not far away, the X-Men catch up to the new mutant who reveals himself to be an extraterrestrial called the Stranger. The people of his species are interested in gene mutation, and thus the Stranger chooses Magneto and Toad as his new specimens, since they insisted on allying themselves with him in the first place. The X-Men can only stand by and watch as their enemies blast off into space. Back home, Cerebro detects the presence of another great power nearby.

2 comments:

  1. Napenda sana jinsi unavyoandika! Asante sana kwa blogu hii!

    ReplyDelete
  2. Online Slot Machines Casino Online | Slots Machines for Real Money
    The top หาเงินออนไลน์ rated online slot machines for your country can be found in the Philippines. And while 제왕 카지노 there are plenty of ways to win at online casinos 온카지노

    ReplyDelete