Thursday, March 1, 2018

Watu-X #8 (The X-Men #8)

Unus Asiyegusika (Unus, the Untouchable)

Hayawani awaacha Watu-X kwa muda mfupi kwa kuwa amechoshwa na kuwalinda wanadamu wanaoogopa na wanaochukia kila mtu mwenye jeni-X. Unus, mgombea mwingine wa kuwa mwanachama wa Undugu wa Vioja Viovu, atembelewa na Bwana Akili. Inabidi ajithibitishe kwa kuwaletea angalau mmojawapo wa Watu-X. Hata hivyo, Unus adanganywa na Hayawani, aliyekuza nguvu zake kwa kutumia mwale wa amplifaya. Mwanzoni, Unus ajifurahisha kwa nguvu zake zilizokuzwa, lakini kisha atambua kwamba hawezi kuzidhibiti. Basi, Watu-X wajitolea kusaidia kuondoa matokeo ya amplifaya hiyo, kwa sharti tu kwamba Unus akatae ombi la kujiunga na Undugu.

The Beast leaves the X-Men briefly since he is fed up with defending the humans who fear and who hate every mutant. Unus, the next candidate for membership in the Brotherhood of Evil Mutants, is visited by Mastermind. He has to prove himself by bringing in at least one X-Man. However, Unus is tricked by the Beast, who amplifies his powers with an amplifier beam. At first Unus welcomes his increased powers, but then he discovers that he is unable to control them. So, the X-Men offer to help reverse the effects of the amplifier, only on the condition that he turn down the Brotherhood's offer to join them.

No comments:

Post a Comment