Ka-Zar na Nchi ya Washenzi (Ka-Zar and the Savage Land)
Hivi karibuni, ilitolewa taarifa kwamba mwanasayansi ameokolewa na mtu mshenzi barani Antaktika, Saiklopsi apanga misheni kwenda Antaktika kuchunguza kama mtu huyo wa mwituni ana jeni-X. Walipofika Antaktika, Watu-X wapeleleza zaidi jangwa lenye theluji karibu na mahali ambapo mtu huyo mshenzi alionekana. Wagundua msitu wa mvua wa kitropiki ndani ya pango kubwa sana lililofichika chini ya barafu. Mara waingiapo, washambuliwa na pterodactyl, wanyama wengine wa kabla ya historia, na pia na Watu wa Vinamasi—kabila la wawindaji wenye uwezo unaozidi ule wa wanadamu ambao hupanda mgongoni mwa wanyama wakubwa wanaofanana na ndege.
Recently, a scientist was reported to have been rescued by a wild man in Antarctica, Cyclops takes charge as leader to set out on a mission to Antarctica to investigate if this jungle man is a mutant. Once in Antarctica, the X-Men go further into the snowy wastelands near where the wild man was spotted. They discover a tropical rain forest in a gigantic cave hidden deep below the ice. Upon entering, they are attacked by pterodactyls, other prehistoric animals, and also by the Swamp Men—a tribe of superior hunters who ride on the backs of giant avian beasts.
Malaika na Msichana Ajabu pia watekwa na hao washenzi, wanaokusudia kuwatoa dhabihu kwa tyrannosaurus. Ili kuwaokoa wanatimu wao waliotekwa, Watu-X wengine waungana na Ka-Zar—mtu wa mwituni, ambaye walikuwa wakimtafuta, na mwenzake Zabu—chui mwenye meno ya kitara. Baada ya pigano fupi dhidi ya Maa-Gor—mtu sokwe, Watu-X na Ka-Zar waenda kijiji cha Watu wa Vinamasi. Kabla tu Malaika na Jean hawajatolewa dhabihu, Ka-Zar aita kundi la mastodoni lisaidie kushinda maadui zake. Mwishoni, Watu-X waondoka, na Ka-Zar aziba kabisa mwingilio uliofichika ambao uliotokea juu ya ardhi.
Both Angel and Marvel Girl are captured by these savages, who intend to sacrifice them to a tyrannosaurus. In order to rescue their captured teammates, the other X-Men ally themselves with Ka-Zar—the jungle man, whom they were seeking, and his companion Zabu—a sabretoothed tiger. After a brief battle against Maa-Gor—the ape man, the X-Men and Ka-Zar go to the Swamp Men's village. Just before Angel and Jean can be sacrificed, Ka-Zar calls a herd of mastodons to come help them defeat their enemies. In the end, the X-Men leave and Ka-Zar permanently seals off the secret entrance that lets out above ground.
Hivi karibuni, ilitolewa taarifa kwamba mwanasayansi ameokolewa na mtu mshenzi barani Antaktika, Saiklopsi apanga misheni kwenda Antaktika kuchunguza kama mtu huyo wa mwituni ana jeni-X. Walipofika Antaktika, Watu-X wapeleleza zaidi jangwa lenye theluji karibu na mahali ambapo mtu huyo mshenzi alionekana. Wagundua msitu wa mvua wa kitropiki ndani ya pango kubwa sana lililofichika chini ya barafu. Mara waingiapo, washambuliwa na pterodactyl, wanyama wengine wa kabla ya historia, na pia na Watu wa Vinamasi—kabila la wawindaji wenye uwezo unaozidi ule wa wanadamu ambao hupanda mgongoni mwa wanyama wakubwa wanaofanana na ndege.
Recently, a scientist was reported to have been rescued by a wild man in Antarctica, Cyclops takes charge as leader to set out on a mission to Antarctica to investigate if this jungle man is a mutant. Once in Antarctica, the X-Men go further into the snowy wastelands near where the wild man was spotted. They discover a tropical rain forest in a gigantic cave hidden deep below the ice. Upon entering, they are attacked by pterodactyls, other prehistoric animals, and also by the Swamp Men—a tribe of superior hunters who ride on the backs of giant avian beasts.
Malaika na Msichana Ajabu pia watekwa na hao washenzi, wanaokusudia kuwatoa dhabihu kwa tyrannosaurus. Ili kuwaokoa wanatimu wao waliotekwa, Watu-X wengine waungana na Ka-Zar—mtu wa mwituni, ambaye walikuwa wakimtafuta, na mwenzake Zabu—chui mwenye meno ya kitara. Baada ya pigano fupi dhidi ya Maa-Gor—mtu sokwe, Watu-X na Ka-Zar waenda kijiji cha Watu wa Vinamasi. Kabla tu Malaika na Jean hawajatolewa dhabihu, Ka-Zar aita kundi la mastodoni lisaidie kushinda maadui zake. Mwishoni, Watu-X waondoka, na Ka-Zar aziba kabisa mwingilio uliofichika ambao uliotokea juu ya ardhi.
No comments:
Post a Comment