Sunday, March 10, 2013

Kipupwe (Winter)

Kipupwe (Winter)
Msimu wa kipupwe (Season of winter)
Majira ya baridi (Cold season)
Solistasi ya kipupwe (Winter solstice)

Kipupwe ndiyo majira ya baridi zaidi ya mwaka, kama majira ya baridi katika hali ya hewa ya wastani. Kipupwe hutokea kati ya demani na masika. Wakati wa solistasi ya kipupwe, mchana huwa mfupi zaidi na usiku huwa mrefu zaidi. Kutokana na theluji, barafu na hali ya hewa nyingine ya kipupwe, baadhi ya ndege huhama; dubu hubumbwaa. Wanyama wengine huweka chakula kwa ajili ya kipupwe ili waweze kuishi, kama vile: kindi, biva, vinyegere, melesi na rakuni. Manyoya ya wanyama wengine hata hubadilika, kwa mfano, manyoya ya mbweha-aktiki hubadilika kuwa meupe kupatana na mandhari ya theluji.
 
"Kipupwe" is the coldest season of the year, like the winter of temperate climates. Kipupwe occurs between autumn and spring. At the winter solstice, the days are shortest and nights are longest. Due to the snow, ice and other wintery weather, some birds migrate; bears hibernate; other animals store food for the winter to live on, such as: squirrels, beavers, skunks, badgers and raccoons; some animals’ fur even changes color, for instance, the arctic fox’s fur changes to white to blend in with the snowy landscape.

No comments:

Post a Comment