Monday, August 25, 2014

Pepo Waliofungiwa Duniani (Earthbound Spirits)

Pepo aliyefungiwa duniani (Earthbound spirit)
Pepo waliofungiwa duniani ni roho za waliokufa ambao wamefungiwa Ardhini na hawawezi kuondoka mpaka wamalize kazi ambayo haijakamilika. Pepo nyingi waliofungiwa Duniani huwa hawakubali kuwa wamekufa. Wao hutokea kwa sababu maalum: kuvuta nadhari kwa kitu kilichopotea, kurekebisha kitu walichofanya vibaya maishani au kuonyesha lililosababisha kifo chao na baada ya jambo hili kusuluhishwa, roho yao itavuka kwenye mwanga, kwa kawaida kwa usaidizi wa mnong’oneza-mizuka au kaimu (aina ya mpunga-pepo).

Earthbound spirits are souls of the dead that are confined to the Earth and cannot leave until completing unfinished business. Many earthbound spirits do not accept that they are dead.  They materialize for a specific reason: to draw attention to something lost, to correct something they did wrong in life or to show the circumstances of their death, and once this matter has been resolved their soul will cross over into the light, usually with the help of a ghost-whisperer or medium (a type of exorcist).

Mizuka-pacha (Doppelgängers)


Mzuka-pacha (Doppelgänger; lit.: Twin ghost)
Mzuka-pacha ni pacha wa nje ya kawaida wa mtu anayeishi, hasa kuwakilisha uovu au bahati mbaya. Katika tamaduni zingine, mzuka-pacha akionekana na marafiki au jamaa wa mtu huyo hutabiri ugonjwa au hatari, ilhali kuona mzuka-pacha wako mwenyewe ni ishara ya mauti.

A doppelgänger is a paranormal double of a living person, typically representing evil or misfortune. In some traditions, a doppelgänger seen by the person’s friends or relatives portends illness or danger, whereas seeing one’s own doppelgänger is an omen of death.

Vardøger
Katika mitholojia ya Kinorsi, mzuka-pacha anaitwa vardøger. Pepo huyu hutangulia mtu anayeishi na huonekana akitekeleza matendo kabla ya wakati wake, na kwa Kifini hujulikana kama etiäinen.

In Norse mythology, a twin ghost is called a vardøger. This spirit precedes a living person and is seen performing their actions in advance, and in Finnish it is known as an etiäinen.

Ka
Katika mitholojia ya Misri Kongwe, ka ilikuwa ”pepo pacha” inayoshikika ikiwa na kumbukumbu na hisia sawa kama mtu asilia.


In Ancient Egyptian mythology, a ka was a tangible “spirit double” having the same memories and feelings as the original person.

Watu-samaki (Fishmen)

Mtu-samaki (Fishman)

Watu-samaki ni wanachama wa mbari ya kiamfibia iliyo karibu kufa ambayo iliishi wakati wa enzi ya Devonia walio na uwezo wa kupumua ndani na nje ya maji. Wao hudhuriwa na rotenoni na nuru ya kung’aa (kutokana na mazingira yao yenye maji machafu), huwa na mikono yenye utando na kucha kali na ngozi ngumu yenye magamba ya kijani-samawati ambayo ikiunganishwa na kipengele chao cha kujiponya huwawezesha kunusurika majeraha ambayo yangekuwa hatari kwa binadamu, kama vile mipigo ya bunduki na kuuliwa kwa kuchomwa. Viumbe hawa huwa na jozi ya mapafu yasiyotumika kwa muda iwapo mayavuyavu yao yataharibika kupita kiasi. 35% ya watu-samaki imetengezwa kwa chembechembe za damu nyeupe zinazokosa kiini. 

Fish-men are members of a nearly extinct amphibious race that lived during the Devonian age, capable of breathing both in and out of water. They are vulnerable to rotenone and bright light (due to their murky water habitat), have webbed hands with sharp claws and tough scaly greenish-blue skin, that with their combined healing factor allows them to survive wounds which would be fatal to humans, such as gunshots and full immolation. These creatures have a dormant set of lungs, in case their gills become irreparably damaged. 35% of fish-people’s blood is composed of white corpuscles lacking a nucleus. 

Kiumbe kutoka Wangwa Mweusi (The Creature from the Black Lagoon)
Kiumbe hiki kutoka wangwa mweusi ndiye mwanachama wa mwisho anayejulikana kuishi katika mbari ya amfibia walio na umbo la binadamu. Mtu-yavuyavu aliyegunduliwa na kupewa jina na Dkt Thompson miaka ya 1930 aliishi katika wangwa ulioko katika eneo pana isiyotafitiwa ya Msitu wa Mvua wa Amazoni. Karibu nusu-karne baadaye, wenyeji wa msitu wa mvua walidai kuwa wameona mtu-samaki mwingine mwenye mapezi ya nyuma mapana yenye rangi ya kaharabu akiishi kwenye maji machafu.

The creature from the black lagoon was the last known surviving member of this race of humanoid amphibians. The gill-man, discovered and named by Dr. Thompson in the 1930s, dwelled in a lagoon located in a largely-unexplored area of the Amazon Rainforest. Almost half a century later, the rainforest natives claimed to have seen another fish-man with large amber-colored dorsal fins inhabiting the murky waters.

Mpanda-farasi Mkosa-kichwa (Headless Horseman)

Mpanda-farasi Mkosa-kichwa (Headless horseman; lit.: Head-lacking horse-rider)

Mpanda-farasi mkosa-kichwa kwa kawaida huendesha gari linalovutwa na farasi akiwa amebeba kichwa chake mkononi mwake na anatwaa mjeledi uliotengezwa kutoka uti wa binadamu. Wakati mpanda-farasi mkosa-kichwa anapoacha kuendesha, kifo hutokea na njia ya pekee ya kuweza kumwogopesha ni kuvaa kifaa cha dhahabu au kurusha kimoja kwenye njia yake.

The headless horseman usually rides a horse-drawn carriage carrying his head under one arm and wielding a whip made from a human spine. When the headless horseman stops riding, a death occurs and the only way he can be frightened away is by wearing a gold object or casting one in his path.

Poltagaisti (Poltergeists)

Poltagaisti (Poltergeist)
Poltagaisti ni onyesho lililo nje ya kawaida la kuwepo au mzuka asiyetambulika, bali mwenye kelele, kuvuruga au kuharibu. Ripoti pia huhusisha vitu visivyo na uhai vikichukuliwa na kutupwa kama na mtu asiyeonekana; kelele kama vile kugonga au hata sauti za binadamu; na mashambulizi madogo ya kimaumbile kwa binadamu, kama vile: kuchuna, kuuma au kupiga.

A poltergeist is a paranormal manifestation of an imperceptible but noisy, disruptive or destructive entity or ghost. Reports also include inanimate objects being picked up and thrown as if by an invisible person; noises such as knocking or even human voices; and petty physical attacks on humans, such as: pinching, biting and hitting.

Wageni wa Anga (Aliens)

Mgeni wa anga (Alien / Extraterrestrial)
Mgeni asiye wa dunia hii, au mgeni wa anga ya nje, ni kiumbe ambacho hakitoki Ardhi. Bunilizi ya kisayansi mara nyingi huwachora wageni wa anga wakiwa na umbo la binadamu au reptilia, ngozi ya kijani-kijivu na kichwa kikubwa chenye umbo la kitunguu, pamoja na viungo vinne. Asili yao kuu ya ubadilishaji ni vyombo vya anga ambavyo vinaweza kusafiri kwa kasi ya kupotosha. Pia wao hujulikana kutengeza miviringo ya mazao, kuwateka binadamu kwa kuwainua ndani ya meli yao kwa mwale wa kusafirisha na kuchunguza kwa undani mapengo ya mwili.

An extraterrestrial alien, or visitor from outerspace, is a being that does not originate from Earth. Science fiction has often depicted aliens with humanoid or reptilian forms, having greenish-gray skin with a large bulbous head, as well as four limbs. Their main source of transportation is spaceships that can travel at warp-speed. They are also known to make crop-circles, abduct humans by beaming them up into their ship and probe their bodily cavities.

Mbari zingine za wageni wa anga (Other alien races)
Mbari za wageni wa anga, kama vile wadudu wa anga, zina uwezo wa kutia mimba mwenyeji kwa yai na wakati kiini tete kimekua, mwenyeji huwa sisimizi wa anga au buibui. Katika makunda wao, hutumia “akili ya mzinga” na kupitisha kumbukumbu kwa wenyeshi wao.

Alien races such as the space bugs, have the ability to impregnate a host with an egg and when the embryo is grown, the host becomes a space ant or spider. Within the brood, they use a “hive mind” to pass memory to their hosts.

Wanyonya-damu (Vampires)

Mnyonya-damu (Vampire)

Wanyonya-damu ni viumbe ambao hujikimu kwa kunyonya damu ya viumbe wanaoishi. Wanyonya-damu huwa na chonge na wanaweza tu kuuawa kwa kuweka wazi kwenye mwanga wa jua au kigingi cha mbao kupitia moyo. Wao pia huchukia sana kitunguu-saumu.

Vampires are beings who subsist by feeding on the blood of living creatures. Vampires have fangs and can only be killed by exposure to sunlight or a wooden stake through the heart. They also really hate garlic.