Thursday, August 9, 2012

Walarasi (Walrus)

Walarasi (pia huitwa Nguva Aktiki au Sili-pembeni mnyama mkubwa wa Bahari ya Aktiki anayefanana na nguva mwenye meno mawili marefu, pia yaitwa pembe, kama tembo.


Mapezi ya mbele
Front flippers
Ngozi
Skin
Pembe
Tusks
Shahamu
Blubber
Sharubu
Whiskers
Sikio
Ear
Tundu za pua
Nostrils
Vifuko vya hewa
Air sacs

Vifuko vya hewa - Vifuko vya hewa chini ya koo shingoni mwa walarasi, shingo lililo fupi na nene, vifuko hivyo vina uwezo wa kuvimba na hewa ili kumpa uwezo wa kuelea wima na kichwa chake juu ya maji. Pia vinatumiwa kama vyumba vya mvumo vinavyotoa sauti kama kengele chini ya maji.

Shahamu - Tabaka ya shahamu kubwa iliyo na upana wa hadi sentimita 15 inayomkinga kutoka kwa baridi.

Masikio - Masikio yao madogo yana kunyanzi ya ngozi nje yao ili kufanya vichwa vyao vinyooke ili waogelee vyema zaidi majini.

Mapezi ya mbele - Kinyume ya mapezi ya nyuma, haya ni marefu kama yaliyo mapana, lakini yana unene na gegedu na vidole vitano kama mapezi ya nyuma. Wanapoogelea, yanatumiwa mara kwa mara kupiga kasia katika mwendo ulio chini lakini mara nyingine hutumiwa kuelekeza.

Ngozi - Ngozi ni ya hudhurungi yenye kunyanzi inayoonekana kama inabadilisha rangi kulingana na halijoto, kwa sababu wakati anapohisi joto, utiririshi wa damu kuelekea usoni mwa ngozi huongezeka ili kumpoza. Tendo hili humpatia walarasi
sura nyekundunyekundu na huonekana kama ana madoadoa. Anapohisi baridi, utiririshi wa damu kuelekea usoni mwa ngozi hupunguzika, kumpatia sura ya kukwajuka.

Pembe - Zimeundwa na dentini, pembe za walarasi ni ndefu sana na ni meno yanayoendelea kukua. Hazitumiwi kuchimbia chakula lakini huwapea usaidizi mwingi wanapojikokota barafuni au ardhini. Pia zinatumiwa kuonyesha utawala na cheo.

Sharubu - Sharubu zao zilizo puani ni nene na zina hali ya juu ya kuhisi na husaidia wanapotafuta chakula.

No comments:

Post a Comment