Monday, August 25, 2014

Watu-Mbweha (Werewolves)

Mtu-Mbweha (Werewolf)
Watu-mbweha ni viumbe wenye sifa za binadamu wanaofanana na mbwa-mwitu ambao husumbuliwa na laikanthropia (uwezo wa kubadilisha umbo kuwa mbwa-mwitu). Mabadiliko haya kwa kawaida husababishwa na kuonekana kwa mwezi mzima. Njia ya pekee ya kuwa mtu-mbweha ni kwa kuumwa na mtu-mbweha mwingine (na kunusurika shambulizi) au kuwekwa chini ya laana (kwa kawaida na mzururaji).

Werewolves are anthropomorphic wolf-like creatures who suffer from lycanthropy (the ability to shapeshift into a wolf). This transformation is generally caused by the appearance of a full moon. The only way to become a werewolf is either to be bitten by another werewolf (and survive the attack) or to be put under a curse (usually by a gypsy).


Baharia Zohali (Sailor Saturn)

Baharia Zohali (Sailor Saturn)
Baharia Zohali anatambulishwa mara ya kwanza anapokuwa rafiki ya Chibi-Usa. Alikuwa mnyamavu asiyeonyesha hisia, mwenye kukomaa upesi akili na mdani, na kusema machache, huwa hapendwi sana na wanafunzi wenzake kwa sababu ya nguvu zake na utekaji wake wa kioja pamoja na mabadiliko yake mengi ya nafsi kutoka kuwa mwenyeji wa Bibi Tisa (kiumbe kiovu kilichoishi ndani yake toka akiwa na miaka 5). 

Sailor Saturn is first introduced when she becomes friends with Chibi-Usa. She was quiet, expressionless, precocious and an introvert, and to say the least, not very popular with her classmates because of her powers and her strange seizures as well as multiple personality changes for being the host of Mistress Nine (the evil entity that lived in her since the age of 5).  

Mabadiliko ya Bibi Tisa (Transformation of Mistress 9)
Baada ya maabara ya babake kulipuka na kuua mamake Hotaru, babake alimwokoa kwa kufanya mwili wake saibentiki na kufanya mkataba na Farao 90.  Kwa kubadilishana, babake alipoteza ubinadamu wake na kuwa mtu mwovu.

After her father’s laboratory exploded, killing Hotaru's mother and critically injuring Hotaru, her father rescued her by making her body cybernetic and made a deal with Pharaoh 90. In exchange, her father lost his humanity and became malevolent. 

Kwa Nguvu ya Sayari ya Zohali (Saturn Planet Power)
Kama askari, Baharia Zohali alimiliki nguvu za ajabu sana za kuharibu, hivi kwamba uamusho wake uliogopwa na Skauti wa Nje; hata hivyo, kwa kutumia nguvu zake kikamilifu ungesababisha kifo chake.

As a Sailor Scout, Sailor Saturn possessed such awesome destructive power that her awakening was feared by the Outer Scouts; however, using her powers to their full extent would bring about her death. 

Ukuta wa Kimya (Silent Wall)
Yeye hutoa nguvu zake zote kutoka mkukishoka wa kunyamaza ambayo inaweza kuunda kizuizi cha kujikinga yeye na wengine dhidi ya mashambulizi ya adui.

She derives all of her powers from her silence glaive that can create a protective barrier around herself and others against enemy attacks. 

Mkukishoka wa Kunyamaza (Silence Glaive)
Shambulizi lake la nguvu zaidi husababisha ukungu mzito ambayo kwanza huwachanganya adui wake wakati ambapo anajitayarisha kwa shambulizi ya ghafla na mradi ncha ya mkukishoka wake inateremshwa hadi ardhini mlipuko wa miali ya nishati ya zambarau humzunguka na kuangamiza eneo linalomzunguka.

Her most power attack produces a thick fog to first disorient her enemy, as she prepares for a surprise attack and once the tip of her glaive is lowered to the ground a radial explosion of purple energy surrounds her and decimates the area around her.

Baharia Uranasi (Sailor Uranus)

Baharia Uranasi (Sailor Uranus)
Baharia Uranasi ni mwenye nguvu zaidi wa Skauti-Baharia wote. Yeye ni mtumiaji kitara stadi, dereva mjuzi wa mashindano ya magari, huwa katika klabu ya riadha na kucheza piano ikiambatana na maonyesho ya fidla ya mpenzi wake. Ingawa yeye ni mzuri zaidi katika darasa lake la kwata, yeye ni mbaya zaidi katika darasa lake la lugha ya Kijapani. Yeye huchukia sana nattou (soya iliyochachuka). 

Sailor Uranus is the strongest of all the Sailor Scouts. She is a skilled fencer, professional racecar driver, belongs to the track-and-field club and plays piano in accompaniment during her lover's violin performances. Although she is best at her physical education class, she is the worst in her Japanese class. She absolutely hates nattō (fermented soybeans). 

Dunia, Tetemeka! (World Shaking!)
Licha ya Uranasi kuwa mungu wa mbingu, Baharia Uranasi anaonekana kuwa na nguvu nyingine za ardhi kama vile shambulizi lake: “Dunia, Tetemeka!” ambayo duara ya dhahabu ya nishati yenye umbo la sayari ya Uranasi hukusanyika kwenye mkono wake huku akibaniza nishati, akitia ufa ardhini kutupa wimbi la kishindo ya utetemeko upande zote. 

Despite Uranus’s being the god of the sky, Sailor Uranus seems to have some earth-based powers as well, such as her attack: “World, Shake!” where a golden sphere of energy shaped like the planet Uranus gathers in her hand as she slams the energy down, cracking the ground beneath her and sending out a seismic shockwave in all directions. 

Upanga wa Anga (Space Sword)
Yeye ndiye hubeba upanga wa anga, mojawapo wa hirizi tatu za kisasili inayobebwa tu na wale walio na fuwele ya moyo safi. Wakati anapoita nguvu za upanga, ubapa wake unaonyooka huwa inang’aa na angezungusha upanga huo ili kutoa mawimbi ya nishati ya dhahabu kuharibu shabaha yake.

She is the bearer of the space-sword, one of the three mythical talismans bore only by those with a pure-heart crystal. When she summons the sword’s power, the extendable blade would glow and she would swing the sword to release of wave of golden energy to destroy the target.

Baharia Neptuni (Sailor Neptune)

Baharia Neptuni (Sailor Neptune)
Baharia Neptuni wakati mwingine huchukuliwa kama asiyeshujaa: mwenye madaha, mstaarabu, wakati mwingine mwenye dharau na anayejitolea kwa dhati katika kazi yake kama Skauti-Baharia. Yeye humiliki nguvu zinazohusishwa na bahari, uwezo wa kubashiri na mengine mengi yanayopewa na kioo cha kichawi. Nguvu zake za utambuzi ni za kiwango cha juu kuliko za wenzake na yanaweza kutofautisha kama fuwele wa moyo safi ni hirizi au la. 

Sailor Neptune is sometimes portrayed as an antihero: elegant, sophisticated, occasionally cold and fully dedicated to her duty as a Sailor Scout. She possesses powers associated with the sea, precognitive abilities and various others granted by a magic mirror. Her powers of perception are greater than those of her teammates and can distinguish whether a pure heart crystal is a talisman or not. 

Kwa Nguvu ya Sayari ya Neptuni (Neptune Planet Power)
Ili kubadilisha, yeye hutumia fimbo ya sayari (inayofanana na rangi ya mdomo). 

To transform, she uses the planet rod (which resembles lipstick). 

Kabobo ya Neptuni (Neptune Tidal Wave)
Anaweza kudhibiti maji na ana udhibiti fulani juu ya bahari. 

She can control water and has some control over the sea itself.

Kioo cha Kina cha Bahari (Deep-Sea Mirror)
Anaweza kufurisha maeneo mazima kwa kabobo, kuzamisha nyumba chini ya maji au kutumia Kioo chake cha Kina cha Bahari kutambua udhaifu wa adui wake.

She can flood entire areas with a tidal wave, submerge a house under water or use her Deep-Sea Mirror to reveal her enemy’s weaknesses.

Baharia Pluto (Sailor Pluto)

Baharia Pluto (Sailor Pluto)
Baharia Pluto ni mwanafizikia na aghalabu huonekana na wenzake kama aliyetengwe na jamii au mpweke; hata hivyo, yeye kwa kawaida huonyesha wema na mapenzi kwa Chibi-Usa (Baharia Mwezi Mdogo). Baada ya kuzaliwa tena, yeye huwa na urafiki zaidi, lakini bado si mwenye mchemuko. Yeye hufanya kazi kama mlinzi wa lango kuu la wakati na anga. Wakati mwingine, yeye huonyesha vitendo vya kuwa na maarifa yote na hudhaniwa kuwa anajua vitendo vyote vya wenzake wake wakati ambapo anapowatazama kutoka kiungo cha wakati na anga. 

Sailor Pluto is a physicist and tends to be seen by her teammates as an outcast or loner; however, she does consistently display warmth and affection for Chibi-Usa (Sailor Mini Moon). After she is reincarnated, she becomes friendlier, but is still not very emotional. She acts as the guardian of the portal of time and space. At times, she displays acts of omniscience and is presumed to be aware of all acts of her teammates as she watches from the nexus of time and space.

Tufe ya Ganeti (The Garnet Orb)
Juu ya mkongojo-ufunguo wake hukaa tufe ya ganeti (hirizi yenye nguvu ambayo humruhusu kufungua mlango wa anga na wakati). 

Atop her keystaff sits the garnet orb (a powerful talisman that allows her to open the space-time door).

Yowe la Wafu (Dead Scream)
Shambulizi analotumia zaidi linaitwa "Yowe la Wafu". Hata hivyo, yeye ndiye skauti-baharia wa pekee ambaye huwa hapigi unyende amri yake ya shambulizi.

Her most used attack is called "Dead Scream". However, she is the only sailor scout who does not scream her attack command.

Kituo cha Wakati (Time Stop)
Kwa nguvu ya hirizi hii, yeye pia anaweza kusimamisha wakati; hata hivyo, hii ni nguvu iliyokatazwa ambayo ilisababisha kifo chake.

With this talisman, she can also stop time; however, this is a forbidden power, which resulted in her death. 

Baharia Mwezi Mdogo (Sailor Mini Moon)

Baharia Mwezi Mdogo (Sailor Mini Moon)
Baharia Mwezi Mdogo ni binti wa baadaye wa Usagi kutoka karne ya kumi na tatu ambaye hutembelea yaliyopita kutafuta usaidizi wa Skauti-Baharia. Ana nywele zilizofungwa nyuma ya rangi ya waridi na macho mekundu. 

Sailor Moon is the future daughter of Usagi from the thirtieth century who visits the past to seek help from the Sailor Scouts. She has pink pigtails and red eyes. 

Mabadiliko ya Bibi Mwovu (Wicked Lady's Transformation)
Anaporudi wakati wa baadaye na Baharia Mwezi, Ukoo wa Mwezi Mweusi hugeuza Mwezi Mdogo kuwa Bibi Mwovu ambaye Mhenga alitumia kasumba na kusuka kumbukumbu zake za familia yake kumfanya afanye anavyoambiwa.

When she returns to the future with Sailor Moon, the Black Moon Clan turns Mini Moon into Wicked Lady, whom Wiseman brainwashed and twisted her memories of her family to make her do his bidding.

Kwa Nguvu ya Mche wa Mwezi (Moon Prism Power)
Anapobadilika kuwa Baharia Mwezi Mdogo, yeye hutumia bweta la mche wa moyo. Wakati anapoita amri yake, bweta lake humetameta na yeye hupota wakati mioyo ya rangi ya waridi hupapatika mwilini mwake kama vipepeo kuunda mavazi yake.

When she transforms into Sailor Mini Moon, she uses the prism heart compact. Once she calls out her command, her compact sparkles and she spins around while pink hearts flutter around her body like butterflies to form her costume.

Baharia Zuhura (Sailor Venus)

Baharia Zuhura (Sailor Venus)
Baharia Zuhura ni wa kwanza kuamshiwa nguvu zake na paka wa mwezi. Ana ndoto siku moja kuwa mtu maarufu anayejulikana. Katika juzuu la tano la mfululizo safu, alikuwa na husudu na Yaten na kumshuku kuwa adui. Yeye hupenda nudo ya ramen, mchuzi wa viungo wenye wali, maua ya "jino la simba" na okidi. 

Sailor Venus is the first to have her powers awakened by a moon cat. She dreams of one day becoming a famous idol. In the fifth volume of the series, she has a crush on Yaten and suspects him of being an enemy. She likes ramen noodles, curry rice, dandelion flowers and orchids. 
  

Mwali wa Hilali (Crescent Beam)
Shambulizi lake dhaifu zaidi ni “Mwali wa Hilali!” ambapo yeye hutupa mwali wa mwanga kwa adui yake.
Her weakest attack is “Crescent Beam!” where she sends a beam of light at the enemy.

Rasharasha ya Miali ya Hilali (Crescent Beam Shower) 
Tafsiri ya nguvu zaidi ya shambulizi hili ilipewa jina “Rasharasha ya Miali ya Hilali!” ambapo miali ya mwanga yalipigwa kwa adui kama rasharasha ya vimondo. 
The stronger version of this attack was named “Crescent Beam Shower!” where multiple beams shot out at the enemy like a meteor shower.

Mfululizo wa Upendo wa Zuhura (Venus Love Chain)
Silaha yake inayomsaidia zaidi ni mfululizo wa upendo ambao yeye hutumia kunyakua, kuteka au kupiga maadui kama mjeledi. 

Her most useful weapon is the love chain which she uses to grab, capture, or hit enemies like a whip.

Kwa Nguvu ya Fuwele ya Zuhura (Venus Crystal Power)
Ili kugeuka kuwa Baharia Mkuu wa Zuhura, yeye hutumia ufito wa fuwele ya kubadilika.

In order to turn into Super Sailor Venus, she uses the crystal change rod.

Shindo la Upendo na Urembo wa Zuhura (Venus Love and Beauty Shock)
Na shambulizi lake la mwisho na la nguvu zaidi ni “Shindo la Upendo na Urembo” ambapo yeye hutupa nishati za dhahabu zenye umbo la moyo kwa mpinzani wake.

And her final and most powerful attack is “Love and Beauty Shock” where she hurls heart-shaped golden energy at her opponent.