Showing posts with label Mimea (Plants). Show all posts
Showing posts with label Mimea (Plants). Show all posts

Sunday, January 27, 2013

Mhadasi (Myrtle)

Mhadasi (Myrtle)
Mihadasi (Myrtles)

Mhadasi (kutoka Kiebrania:  הדס hadas) ni jenasi ya spishi moja au mbili za mimea inayochanua katika familia ya Myrtaceae, inayopatikana kusini mwa Ulaya na kaskazini mwa Afrika. Mmea huo ni mti mdogo au kichaka chenye majani mwaka mzima ambacho hukua hadi mita 5 kwa urefu. Matunda yake ni beri ya mviringo yenye mbegu nyingi za buluu nyeusi.

The myrtle (from Hebrew: הדס hadas) is a genus of one or two species of flowering plants in the Myrtaceae family, found the south of Europe and the north of Africa. The plant is a small evergreen tree or bush that grows up to 5 meters tall. Its fruits are round berries with many dark blue seeds.

Saturday, January 26, 2013

Mhazeli (Hazelnut tree)

Mhazeli (Hazelnut tree)
Mihazeli (Hazelnut trees)
Hazeli (Hazelnut)

Hazeli (kutoka Kijerumani: Hasel) ni njugu ya mhazeli ulio aina ya mti wa familia ya mbetula ulio na majani yenye meno na umbo la mviringo ambayo huzaa njugu za kulika.

The hazelnut (from German: Hasel) is the nut of the hazel which is a type of tree of the birch family having toothed and round leaves that bear edible nuts.

Mrowani (Rowan)

Mrowani (Rowan tree)
Mirowani (Rowan trees)

Mrowani, pia huitwa mjivujivu-milima, ni aina ya mti wenye majani yenye umbo la unyoya na vishada vya beri nyekundu kali.

The rowan, also called the mountain ash-tree, is a type of tree with pinnate leaves and clusters of bright red berries.

Mwerebi (Willow)


Mwerebi (Willow; Salix) (ערבה 'aravah)
Mwerebi mliaji (Weeping willow; Salix babylonica)

Mwerebi (kutoka Kiebrania: ערבה 'aravah) ni mti umeao karibu na maji na unaojulikana kwa majani yake membamba yenye umbo la fumo na vishada vya maua madogo yaliyosongamana, spishi nyingi huwa na vitawi vigumu vinavyopindika kwa urahisi vinavyotumika kutengeza vichanja.

The willow (from Hebrew: ערבה 'aravah) is a tree that grows near water and known for its narrow, lance-shaped leaves and dense catkins, many species have tough, pliable twigs used for making wickerwork.

Mwaramoni (Chestnut tree)

Mwaramoni (Chestnut tree)
Miaramoni (Chestnut trees)
Aramoni (Chestnut)

Aramoni (kutoka Kiebrania: ערמון 'armun) ni njugu ya mwaramoni ulio mti wa kupukutika majani unaofanyiza jenasi Castanea ya familia ya mfune ulio na majani yenye meno na umbo la mstatili na huzaa njugu za kulika zilizozungushiwa ndani ya kichomanguo.
 
The chestnut (from Hebrew: ערמון 'armun) is the nut of a chestnut tree which is a deciduous tree constituting the genus Castanea of the beech family having toothed and oblong leaves and bear edible nuts enclosed inside a bur.

Friday, January 25, 2013

Mteashuri (Larch)

Mteashuri (Larch)
Miteashuri (Larches)

Miteashuri (kutoka Kiebrania: תְּאַשּׁוּר ţe'ashur) ni mikoni katika jenasi ya Larix ya familia Pinaceae. Hutofautiana kwa ukubwa kuanzia mita 20 hadi 45. Inapatikana nusudunia ya kaskazini hasa misituni mwa Urusi na Kanada.
 
Larches (from Hebrew: תְּאַשּׁוּר ţe'ashur) are conifers in the genus Larix of the Pinaceae family. They vary in size from 20 to 45 meters. They are found in the northern hemisphere especially in the forests of Russia and Canada.

Aina za Miti (Types of Trees)


Aina za miti (Types of trees)

Mbetula Birch
Mchikichi Palm tree
Mfune Beech tree
Mjozi Walnut tree
Mpopla Poplar
Mseda Cedar
Mshira Maple
Msprusi Spruce
Mteashuri Larch
Mwaloni Oak
Mwerebi Willow
Mwerezi Lebanon cedar

Monday, September 24, 2012

Mshira (Maple)

Mshira (Maple tree; Acer)

Mishira hupandwa kama kivuli au miti ya mapambo inayomea nchi za kaskazini, kutoa mbao au hutumiwa kutengeneza shira au sukari. Majani ya mshira ni mekundu au dhahabu wakati wa majira ya mavuno.
Maple trees are grown as shade or ornamental trees which grow in northern countries, for timber or used to make syrup or sugar. Maple leaves are red or gold in autumn.

Monday, May 28, 2012

Mpekani (Pecan)

Mpekani (Pecan tree; Carya illinoinensis)

Mpekani ni aina ya mhikoria mrefu unaopatikana Kusini mwa nchi za Marekani na Meksiko ambao hukuzwa kwa njugu zake tamu za kulika zalizo na makaka laini yenye umbo la yai na hutumika kutengeza pai za pekani.
The pecan tree is a type of tall hickory found in the southern US and Mexico that is grown for its oval, smooth-shelled, sweet edible nuts and used in making pecan pies.

Mwelmu (Elm)

Mwelmu (Elm tree; Ulmus)
Mwelmu wa Amerika (American elm; Ulmus americana)

Mwelmu ni mti unaojulikana kwa matawi yake yanayomea yakitambaa. Ganda la mwelmu lililokatwa kwa vipande na kuchemsha liliwasitiri wakazi wa mashambani nchini Unorwe wakati wa njaa kubwa mwaka wa 1812.
The elm is a tree known for its branches which grow in a spreading manner. Elm bark, cut into strips and boiled, sustained the rural population of Norway during the great famine of 1812.

Tuesday, May 24, 2011

Muundo wa Seli ya Mmea (The Structure of a Plant Cell)

Muundo wa seli ya mmea (The structure of a plant cell)

Chembe cha wangaStarch granule
Dutuvuo (Mitokondria)Mitochondrion
KiiniNucleus
Kiini kidogoNucleolus
Kitone cha asidi za shahamuLipid droplet
KitunduPore
Kiungo cha lamela za katiCompound middle lamella
KloroplastiChloroplast
Lamela ya katiMiddle lamella
LukoplastiLeucoplast
Nafasi kati ya seliIntercellular space
OganeliOrganelle
Oganeli ya GolgiGolgi apparatus
PeroksisomuPeroxisome
PlazmodesmaPlasmodesma
Retikulamu laini ya utegili wa ndaniSmooth endoplasmic reticulum
Retikulamu ya kukwaruza ya utegili wa ndaniRough endoplasmic reticulum
RibosomuRibosome
Seli ya mmeaPlant cell
Ukuta wa seliCell wall
Ukuta wa seli wa msingiPrimary sell wall
Utando wa kiiniNuclear envelope
Utando wa seliCell membrane
Utegili wa njeEctoplasma
Utegili wa seliCytoplasm
VakuoliVacuole

Maumbo ya Majani (Shapes of Leaves)



Maumbo ya Majani (Shapes of Leaves)

Umbo la figo Reniform
Umbo la kiganja Palmate
Umbo la klova Trifoliolate
Umbo la mkuki Lanceolate
Umbo la moyo Cordate
Umbo la mshale Hastate
Umbo la mstari Linear
Umbo la mviringo Orbiculate
Umbo la mwiko Spatulate
Umbo la ngao Peltate
Umbo la unyoya Pinnatifid
Umbo la unyoya shufwa Even-pinnate
Umbo la unyoya witiri Odd-pinnate
Umbo la yai Ovate 

Monday, May 23, 2011

Makali ya Majani (Leaf margins)

Makali ya majani (Leaf margins)

Umbo la ndeweLobate
Jani lenye makali mororoSmooth-edged leaf 
Jani lenye vinywele Ciliate leaf
Umbo la menoDentate
Umbo la meno ya mviringoCrenate
Umbo la menomenoDoubly dentate