Baharia Zebaki (Sailor Mercury)
Baharia
Zebaki alikuwa Skauti-Baharia wa kwanza aliyejiunga na Baharia Mwezi katika
mapigano dhidi ya Ufalme wa Giza. Yeye huwa mfanya-mikakati wa Baharia-Askari
wa Ndani na hutumia tarakilishi ya mikono kama skana na kichanganua-data. Rangi
anayoipenda zaidi ni samawati. Hupenda kusoma, kucheza sataranji na kuogelea.
Vyakula anavyovipenda zaidi ni sandwichi na anmitsu (jeli iliyotengenezwa kwa mwani mwekundu na
maharagwe ya azuki). Chakula asichokipenda ni bangala mkia-manjano.
Mashambulio
Shambulio
lake la kwanza linaitwa “Viputo vya Zebaki!” (kwa Kiingereza: Mercury
Bubbles Blast!; Kijapani: Bubble Spray!). Shambulio hili hutengeneza
ukungu ambao humpofusha adui.
Her first attack is called "Mercury Bubbles!" (in English: Mercury Bubbles Blast!; Japanese: Bubble Spray!). This attack produces fog that blinds the enemy.
No comments:
Post a Comment