Monday, October 8, 2012

Trolu (Trolls)

Trolu (Troll / Trolls)

Mazimwi ya Kiskandinavia huitwa trolu; lakini tofauti na mazimwi ya kawaida, trolu hawawezi kubadilisha umbo. Trolu ni kiumbe kisicho cha dunia hii katika mitholojia ya Kinorsi na hadithi za jadi za Kiskandinavia. Trolu kwa kawaida huishi kwenye miamba, milima na mapango, na huishi pamoja katika familia ndogo na ni nadra kuwa na manufaa yoyote kwa binadamu. Trolu huelezwa kama wazee kupita kiasi, wenye nguvu sana, lakini waenda pole na wajinga, na mara nyingi huelezwa kama wala-watu na hugeuka jiwe wanapowekwa wazi kwa mwanga wa jua.

Scandinavian goblins are called trolls; however unlike regular goblins, trolls cannot shape-shift. A troll is a supernatural being in Norse mythology and Scandinavian folk-tales. Trolls normally dwell in rocks, mountains, or caves, and live together in small families and are rarely of any use to humans. Trolls are described as being extremely old, very strong, but slow and dim-witted, and are at times described as man-eaters and turn to stone upon exposure to sunlight.

-a Kiskandinavia (Scandinavian)
mwamba (rock)
pango (cave)
-zee (old)
-enye nguvu (strong)
-jinga (dumb)
mla-watu (man-eater)
mwanga wa jua (sunlight)

Mazimwi (Goblins)

Zimwi (Goblin)
Mazimwi (Goblins)

Zimwi ni kiumbe kiovu au kitundu cha kihekaya ambacho kwa kawaida huwa cha kioja kilicho na uwezo wa kujigeuza kuwa maumbo mbalimbali na anaaminiwa kuwa na madhara kwa binadamu na huishi katika misitu mikubwa. Yanadhaniwa kuwa na uwezo, tabia na sura mbalimbali kutegemea hadithi na nchi asilia. Wakati mwingine, mazimwi huorodheshwa kama viumbe vinavyoudhi wakati wote na kwa kiasi yana uhusiano na brauni na nomu . Kwa kawaida huchorwa kuwa kimo cha kijeba . Mara nyingi pia husemekana kuwa na uwezo mbalimbali wa kichawi.
 


The goblin is a legendary evil or mischievous creature, that is usually grotesque with the ability to change into various forms and is believed to be harmful to humans and live in large forests. They are believed to have various abilities, temperaments and appearances depending on the story and country of origin. In some cases, goblins are classified as constantly annoying creatures and somewhat are related to the brownie and gnome. They are usually depicted to be the size of a dwarf. They are often said to possess various magical powers.

-a kihekaya (legendary)
kuudhi (to annoy)
kijeba (dwarf)
-a kichawi (magical)

Monday, September 24, 2012

Mamalia wasio na meno (Edentata)

Mamalia wasio na meno (Edentata)
Mamalia asiye na meno (Toothless mammal)

Armadilo Armadillo
Kakakuona Pangolin
Mhanga Aardvark
Mla-sisimizi Anteater
Slothi Sloth
Tamandua Tamandua

Mshira (Maple)

Mshira (Maple tree; Acer)

Mishira hupandwa kama kivuli au miti ya mapambo inayomea nchi za kaskazini, kutoa mbao au hutumiwa kutengeneza shira au sukari. Majani ya mshira ni mekundu au dhahabu wakati wa majira ya mavuno.
Maple trees are grown as shade or ornamental trees which grow in northern countries, for timber or used to make syrup or sugar. Maple leaves are red or gold in autumn.

Thursday, August 9, 2012

Mamalia wa Bahari (Marine Mammals)

Oda ya nyangumi (Cetacea)
Wanyama wenye miguu-mapezi (Pinnipedia)
Pinipedi (Pinniped)


Beluga Beluga
Narwali Narwhal
Nguva (Manatii) Dugong (Manatee)
Nyangumi buluu Blue whale
Nyangumi-kibyongo Humpback whale
Nyangumi-spemaseti Sperm whale
Orka (Nyangumi-muuaji) Orca (Killer whale)
Pomboo Dolphin
Poposi Porpoise
Sili Seal
Sili-manyoya Fur seal
Simba-bahari Sea lion
Tembo-bahari Elephant seal
Walarasi Walrus

Walarasi (Walrus)

Walarasi (pia huitwa Nguva Aktiki au Sili-pembeni mnyama mkubwa wa Bahari ya Aktiki anayefanana na nguva mwenye meno mawili marefu, pia yaitwa pembe, kama tembo.


Mapezi ya mbele
Front flippers
Ngozi
Skin
Pembe
Tusks
Shahamu
Blubber
Sharubu
Whiskers
Sikio
Ear
Tundu za pua
Nostrils
Vifuko vya hewa
Air sacs

Vifuko vya hewa - Vifuko vya hewa chini ya koo shingoni mwa walarasi, shingo lililo fupi na nene, vifuko hivyo vina uwezo wa kuvimba na hewa ili kumpa uwezo wa kuelea wima na kichwa chake juu ya maji. Pia vinatumiwa kama vyumba vya mvumo vinavyotoa sauti kama kengele chini ya maji.

Shahamu - Tabaka ya shahamu kubwa iliyo na upana wa hadi sentimita 15 inayomkinga kutoka kwa baridi.

Masikio - Masikio yao madogo yana kunyanzi ya ngozi nje yao ili kufanya vichwa vyao vinyooke ili waogelee vyema zaidi majini.

Mapezi ya mbele - Kinyume ya mapezi ya nyuma, haya ni marefu kama yaliyo mapana, lakini yana unene na gegedu na vidole vitano kama mapezi ya nyuma. Wanapoogelea, yanatumiwa mara kwa mara kupiga kasia katika mwendo ulio chini lakini mara nyingine hutumiwa kuelekeza.

Ngozi - Ngozi ni ya hudhurungi yenye kunyanzi inayoonekana kama inabadilisha rangi kulingana na halijoto, kwa sababu wakati anapohisi joto, utiririshi wa damu kuelekea usoni mwa ngozi huongezeka ili kumpoza. Tendo hili humpatia walarasi
sura nyekundunyekundu na huonekana kama ana madoadoa. Anapohisi baridi, utiririshi wa damu kuelekea usoni mwa ngozi hupunguzika, kumpatia sura ya kukwajuka.

Pembe - Zimeundwa na dentini, pembe za walarasi ni ndefu sana na ni meno yanayoendelea kukua. Hazitumiwi kuchimbia chakula lakini huwapea usaidizi mwingi wanapojikokota barafuni au ardhini. Pia zinatumiwa kuonyesha utawala na cheo.

Sharubu - Sharubu zao zilizo puani ni nene na zina hali ya juu ya kuhisi na husaidia wanapotafuta chakula.

Makazi ya Walarasi (The Habitat of the Walrus)

Makazi (The habitat)
Walarasi (Walrus)
Walarasi wa Pasifiki (The Pacific walrus)
Walarasi wa Laptevu (The Laptev walrus)
Walarasi wa Atlantiki (The Atlantic walrus)

Walarasi wa Pasifiki wanaishi Baharini mwa Beringi na Chukchi.

Walarasi wa Laptevu wanaishi Baharini mwa Laptevu.

Walarasi wa Atlantiki wanaishi maeneo ya Grinlandi na Kanada.